Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wanachama wachangishana Yanga, wataka Sh1.5 Bilioni

Muktasari:

Mei 18 itafanyika halfa rasmi ya kukusanya fedha kwa ajili ya kuisaidia klabu hiyo kufanya usajili pamoja na kujiendesha

Dar es Salaam. Wanachama wa Yanga waendelea kuichangia timu yao muda mfupi kabla ya mchakato wa kupiga kura huku lengo likiwa kukusanya Sh 1.5 Bilioni.

Mwenyekiti wa kamati ya hamasa na michango ya Yanga, Anthony Mavunde alisema mkakati uliokuwepo ni kukusanya Sh1.5 Bilioni na mchakato wa kukusanya utafungwa Mei 18.

Alisema Kamati yao ilikuwa na mpango muda mfupi na kufafanua kwamba Yanga haiombi inachangisha kupitia wanachama.

Kabla ya uchaguzi kuanza, Mavunde alichukua jukumu la kuchangisha kuelekea kwenye mechi ya kesho huku Mavunde akifungua kwa kuchangia Sh 1 Milioni.

Kuchangia kuliendelea kwenye Meza kuu ambapo Lucas Mashuri, Kifukwe, Sam Mapande walichangia Sh1 Milioni kila mmoja.

George Mkuchika alitoa Sh 2 Milioni na Tindwa Beda alitoa Sh 1.5, Ally Mchungahela alitoa Sh 250,000,  Seif Gulamali alitoa Dola 200  huku lengo likiwa kukusanya Sh 10 Milioni kwa Meza kuu.

Akizungumzia mchakato wa uchangishaji, Mavunde alisema:"Tumetengeneza kadi 1500 kila moja ina thamani ya Sh 1 Milioni, tumezigawa kwa makundi na mtu mmoja mmoja.

"Zoezi la limeanza muda mrefu na hamasa ni kubwa, hivyo Mei 18 katika hoteli ya Serena tutakuwa na fundraising kwa ajili ya michango kabla ya zoezi kufungwa na kukabidhi michango kwa uongozi.

Alisema kusudio la Mei 18 ni kukusanya zaidi ya Milioni 500 kabla kufungwa siku hiyo.