Wanachama 48 wajitosa uchaguzi Simba
Muktasari:
- Kati ya watia nia hao 48, saba ni wa nafasi ya Uenyekiti na watia nia 41 wanataka kugombea nafasi tano za ujumbe wa Bodi ya Wakurugenzi.
WATIA nia 48 wamejitokea kuchukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi wa Klabu Simba katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Januari 30, 2027, huku wakitumia jumla ya shilingi milioni nane laki mbili na nusu.
Kati ya watia nia hao 48, saba ni wa nafasi ya Uenyekiti na watia nia 41 wanataka kugombea nafasi tano za ujumbe wa Bodi ya Wakurugenzi.
Taarifa iliyotolewa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) jana Jumamosi, Novemba 21, 2026 imewataja watia nia saba wa nafasi ya Uenyekiti kuwa ni Anindum Semu, Geofrey Nyange, Mohamed Soloka, Murtaza Mangungu, Dk. Seif Muba, Selemani Haroub katika eneo hili anatakiwa kushinda mtu mmoja pekee.
Mangungu ambaye kulikuwa na usiri mkubwa kuhusu kuchukua kwake fomu anaomba kutetea tena nafasi hiyo. Fomu ya kugombea Uenyekiti ilikuwa inatolewa kwa shilingi 300,000, hivyo wanachama hao wametoa jumla ya shilingi milioni 2,100,000 (milioni mbili na laki moja)
Wanaowania nafasi tano za Ujumbe wa Bodi ni Aaron Mrina, Abdallah Mgomba, Alfred Elia, Arnold Nzali, Aziz Kaku, Andrew Tupa, Christopher Kabalika, Damian Manembe, Eli Paulo na Enock Bwigane,
Pia kuna Fadhili Famonga, Farid Tamim, Francis Ndulane, Hamisi Tika, Hassan Kakayoo, Hussein Simba, Isabela Faya, Issa Masoud, Jamhuri Kihwelo na Jonathan Nkya.
Wapo pia Juma Pinto, Laurian Mganga, Mariam Ibrahim, Mariam Shemzigwa, Mohamedi Hamisi, Omari Mazola, Pendo Mapugio, Rachel Chagonja, Raphael Chegeni, Richard Sukia, Rodney Chiduo, Said Tully, Said Njechele, Saleh Afif, Salum Hamidu, Salim Maftah, Shukuru Mtego, Dk. Suleiman Selrera, Ussi Pondeza, Wolfred Nyamwija na Yusuph Yenga.
Kwa mujibu wa taarifa ya kamati ya uchaguzi fomu hii ilikuwa inatolewa kwa kiasi cha shilingi 150,000, hivyo zimekusanywa shilingi 6,150,000 (milioni sita na laki moja na nusu) hivyo jumla fomu zote zimechukuliwa kwa shilingi milioni nane, laki mbili na nusu.
Kwa mujibu wa kalenda ya Uchaguzi wa klabu hiyo, kuanzia Novemba 25 hadi Novemba 26, 2026 ni uhakiki wa fomu zilizorejeshwa na uhakiki wa sifa za wagombea.
Uchaguzi wa Simba ambao kikatiba unatakiwa kufanyika kila baada ya miaka minne umepangwa kufanyika Januari 30, 2027.