Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wamiliki wa klabu za soka England waliokumbwa na kashfa

Muktasari:

  • Makala hii inawazungumzia matajiri waliowahi kuwekeza kwenye soka la England kwa kutumia fedha nyingi kabla ya kukumbwa na kashfa za ufujaji na mambo mengineyo yaliyowafanya kuishia vifungoni.

LONDON, ENGLAND

MMILIKI wa klabu ya soka ya Birmingham City ya England, Carson Yeung, ametupwa jela huko Hong Kong baada ya kukutwa na hatia ya ufujaji fedha.

Lakini, bilionea huyo si mtu wa kwanza aliyewahi kujihusisha na soka la England kuwahi kukumbwa na kashfa za ufujaji fedha katika nchi zao. Hiyo ni baada ya kuwekeza kwenye soka la England.

Makala hii inawazungumzia matajiri waliowahi kuwekeza kwenye soka la England kwa kutumia fedha nyingi kabla ya kukumbwa na kashfa za ufujaji na mambo mengineyo yaliyowafanya kuishia vifungoni.

Thaksin Shinawatra

Bilionea huyo mwanasiasa nchini Thailand, alinunua hisa zenye thamani ya Pauni 81.6 milioni na hivyo kuwa mmiliki wa Manchester City mwaka 2007, licha ya kwamba kwao alikuwa akikabiliwa na kesi ya rushwa.

Kulikuwa na wasiwasi mkubwa kuhusiana na pesa zake na matumizi ya mali za umma. Uchunguzi uliofanywa dhidi yake haukuchukua muda mrefu na mahakama ya Thailand iliamua kubinafsisha mali za bilionea huyo zilizokuwa na thamani ya Dola 1.4 bilioni.

Vikundi vya Haki za Binadamu vilikosoa mpango wa Shinawatra wa kuinuanua Manchester City, kabla ya bilionea huyo kuondolewa madarakani kwa nguvu ya jeshi baada ya kudaiwa kutumia vibaya madaraka.

Mwishoni mwa mwaka 2007, Shinawatra alifunguliwa mashitaka pamoja na mkewe Pojaman na Pombejra na kufungwa miaka miwili jela.

Licha ya mambo hayo kutokea, bilionea huyo bado ni mjumbe kwenye bodi ya Man City. Mwaka 2009, Man City ilimwondoa Shinawatra katika nafasi ya Rais wa Heshima wa klabu hiyo. Bilionea huyo baadaye alimtaliki mkewe na kwenda kuishi uhamishoni Dubai.

Owen Oyston

Owen Oyston, bilionea mmiliki wa klabu ya Blackpool alifungwa jela kwa kesi ya kubaka mwaka 1996. Mfanyabiashara huyo mwenye pesa za kutosha, alianza kuimiliki Blackpool FC Mei 1988 baada ya kupata pesa kufuatia kuuza mashamba ya familia yake.

Utajiri wake uliifanya klabu ya Blackpool kuwa imara zaidi na hivyo kupanda hadi kwenye Ligi Kuu England na kuonyesha upinzani mkali.

Lakini, mwaka 1996 alifungwa jela baada ya kubaka binti wa miaka 16 huko nyumbani kwake mjini Lancashire. Mke wake, Vicki alichukua madaraka ya kuwa Mwenyekiti wa klabu hadi aliporithiwa na mtoto wao wa kiume, Karl mwaka 1999.

Oyston aliruhusiwa kutoka jela baada ya kutumikia nusu ya kifungo chake na kuendelea na biashara zake.

Bado anamiliki klabu ya Blackpool kutokana na kuwa na hisa nyingi, lakini hakuwahi kutokea hadharani kwenye klabu hiyo hadi ilipofika mwaka 2002 wakati walipozindua majukwaa mawili katika uwanja wa timu hiyo.

Freddy Shepherd

Licha ya kwamba hakujihusisha kwenye kashfa ya rushwa au uhalifu wowote, Mwenyekiti huyo wa klabu ya Newcastle United na aliyekuwa msaidizi wake, Douglas Hall, walilazimika kujiuzulu baada ya kuripotiwa kuwahi kuwatusi mashabiki wanawake wa klabu hiyo kuwa ni sawa na mbwa.

Mwandishi wa Habari za uchunguzi, Mazher Mahmood, ambaye anafahamika kama ‘Sheikh feki’, aliwanasa wawili hao na kuwarekodi wakiwashambulia mashabiki wa kike wa klabu hiyo pamoja na straika, Alan Shearer.

Baada ya kuibuka kwa ripoti hiyo, mashabiki wa Newcastle na wajumbe wengine wa bodi walikasirika na hivyo kuwataka wajiuzulu. Lakini, Shepherd na Hall bado wanamiliki hisa katika klabu hiyo. Julai 2007, Shepherd aliyekuwa Mwenyekiti wa Heshima aling’atuka kutokana na afya yake kuzorota na hivyo kumuuzia hisa zake bilionea mchuuzi wa vifaa vya michezo, Mike Ashley.