Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vardy wa Zenji anukia Mashujaa

VADI Pict

Muktasari:

  • Vardy aliibuka mfungaji bora wa Ligi ya Zanzibar akiwa na kikosi cha KVZ FC, baada ya kufunga mabao 21 katika mechi zake 29, alizocheza kwa msimu mzima wa 2025-2026, huku akitoa pia asisti nane na kumfanya kuhusika kwenye jumla ya mabao 29.

Mashujaa iko katika hatua za mwisho za kukamilisha usajili wa mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Zanzibar (ZPL) kwa msimu wa 2025-2026, Michael Joseph ‘Vardy’ baada ya kikosi hicho cha maafande kufikia makubaliano rasmi na nyota huyo.

Vardy aliibuka mfungaji bora wa Ligi ya Zanzibar akiwa na kikosi cha KVZ FC, baada ya kufunga mabao 21 katika mechi zake 29, alizocheza kwa msimu mzima wa 2025-2026, huku akitoa pia asisti nane na kumfanya kuhusika kwenye jumla ya mabao 29.

Kiwango bora cha nyota huyo kiliiwezesha KVZ FC kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Zanzibar, baada ya kumaliza na pointi 67, ikifuatiwa na JKU SC iliyomaliza ya pili na pointi 64 kwa msimu wa 2025-2026, jambo lililoivutia Mashujaa kuitaka saini yake.

Mwanaspoti linatambua nyota huyo alikuwa katika mazungumzo na timu za Namungo FC, Coastal Union na Pamba Jiji, ambazo zote zilionyesha nia ya kuipata saini yake, japo Mashujaa imekuwa mstari wa mbele na sasa mazungumzo yamefikia pazuri.

Akizungumza na Mwanaspoti, Mwenyekiti wa Mashujaa, Meja Abdul Tika amesema wameshapokea ripoti ya benchi la ufundi kwa ajili ya kufanyia maboresho mbalimbali katika kikosi hicho cha maafande, ingawa hadi sasa hakuna usajili uliokamilika.

“Kwa sasa tunataka kwanza kukamilisha suala la kumpata kocha mkuu mpya baada ya kuondoka kwa Jamhuri Kihwelo ‘Julio’, muda wowote kuanzia sasa tutakamilisha baadhi ya taratibu hizo kwa sababu yapo mazungumzo yanaendelea,” amesema Tika.

Idadi hiyo ya mabao 21 aliyofunga Vardy baada ya kuichezea KVZ FC kwa dakika 2320 kwa msimu wa 2025-2026, ni sawa na aliyoyafunga mshambuliaji, Abdallah Iddi ‘Pina’ akiichezea Mlandege FC, kwa msimu wa 2024-2025 na kuivutia Pamba Jiji.

Msimu wa 2024-2025, katika Ligi Kuu ya Zanzibar, Pina aliibuka mfungaji bora baada ya kufunga mabao 21, kwenye mechi 22, alizocheza Mlandege FC, huku akichangia pia mengine 12 (asisti).

Licha ya kutabiriwa makubwa na Pamba Jiji msimu wa 2025-2026, Pina alishindwa kufanya vizuri kutokana na kuandamwa na majeraha na dirisha dogo la Januari mwaka 2025, aliachana na timu hiyo na kurudi visiwani Zanzibar na kujiunga na kikosi cha Muembe Makumbi City.