Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ujerumani ilivyoiduwaza Argentina fainali Kombe la Dunia 2014

Muktasari:

  • Ujerumani iliiadhibu Argentina bao 1-0 katika muda wa nyongeza 120 likiwekwa wavuni na Mario Gotze zikiwa zimebaki dakika saba ngwe hiyo kukamilika.

Timu ya Taifa ya Ujerumani ndio mabingwa wa Kombe la Dunia mwaka 2014 wakichukua taji hilo kwa mara ya nne katika historia ya mashindano hayo.


Ujerumani iliiadhibu Argentina bao 1-0 katika muda wa nyongeza 120 likiwekwa wavuni na Mario Gotze zikiwa zimebaki dakika saba ngwe hiyo kukamilika.


Mchezo huo ulipigwa Maracana Rio de Janeiro nchini Brazil. Nyota huyo alithibitisha ubora wake mbele ya wachezaji wa Argentina, huku akiiongezea taji la nne ukijumlisha na yale ambayo imetwaa mwaka 1954, 1974 na 1990.


Ujerumani ilichukua kibabe kombe hilo mbele ya nyota wa Argentina wakimo Lionel Messi, Pablo Zabaleta na Philipp Lahm.