Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Abdulmajid Mangalo atimkia Mashujaa

MANGALO Pict

Muktasari:

  • Mabosi wa Mashujaa FC wameboresha eneo hilo baada ya aliyekuwa beki tegemeo wa kikosi hicho cha maafande, Mohamed Mussa kujiunga na mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara Klabu ya Yanga, kuitumikia msimu wa 2026-2027.

ALIYEKUWA beki wa kati wa Pamba Jiji, Abdulmajid Mangalo amekamilisha usajili wake Mashujaa FC kwa mkataba wa miaka miwili, akienda kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Mo-hamed Mussa aliyejiunga na Yanga.

Mabosi wa Mashujaa FC wameboresha eneo hilo baada ya aliyekuwa beki tegemeo wa kikosi hicho cha maafande, Mohamed Mussa kujiunga na mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara Klabu ya Yanga, kuitumikia msimu wa 2026-2027.

Akizungumza na Mwanaspoti, Mwenyekiti wa Mashujaa, Meja Abdul Tika amesema tayari kuna wachezaji wamefikia makubaliano ya kujiunga na kikosi hicho cha maafande na muda wowote kuanzia sasa wataanza kuwatangaza mmoja baada ya mwingine.

“Baada ya kukamilisha taratibu za kumpata kocha mpya kwa sasa tumehamishia nguvu katika wachezaji wapya pia, mazungumzo yanaendelea vizuri na kuanzia wiki inayoanza kesho Juma-tatu Julai 27, 2026, tutaanza kuwatangaza rasmi,” amesema Tika.

Hata hivyo, licha ya kauli ya Tika ila Mwanaspoti linatambua Mangalo amejiunga na timu hiyo kwa mkataba wa miaka miwili, baada ya kandarasi yake ya mwaka mmoja na Pamba Jiji ali-yojiunga nayo Agosti 7, 2025, akiwa ni mchezaji huru kumalizika.

Beki huyo alijiunga na Pamba Jiji na kuungana tena na aliyekuwa kocha wake, Mkenya Francis Baraza aliyefanya naye kazi wakiwa Biashara United na alijiunga na kikosi hicho cha ‘TP Lindanda’ au ‘Wanakawekamo’, akiwa mchezaji huru.

Mangalo alijiunga na Pamba Jiji ikiwa ni pendekezo la Kocha Mkuu, Francis Baraza licha ya nyota huyo kukaa nje kwa msimu mzima wa 2024-2025, kutokana na kusumbuliwa na maje-raha ya goti aliyoyapata akiwa na kikosi cha Singida Fountain Gate.