Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Twiga Stars yaitandika Botswana kufuzu Olympic

Muktasari:

  • Kipindi cha kwanza kilikuwa cha vuta-nikuvute huku timu zote zikicheza kwa tahadhari kubwa ili kutokubali bao la mapema.

TIMU ya Taifa ya Wanawake ya Tanzania, 'Twiga Stars', imeanza vyema safari  ya kusaka tiketi ya kushiriki Michezo ya Olimpiki ya Los Angeles 2028 baada ya kuondoka na ushindi wa bao 1-0 ugenini dhidi ya wenyeji Botswana mechi iliyopigwa Uwanja wa Taifa wa Botswana jijini Gaborone.

Kipindi cha kwanza kilikuwa cha vuta-nikuvute huku timu zote zikicheza kwa tahadhari kubwa ili kutokubali bao la mapema.

Wenyeji Botswana walijaribu kutumia kasi ya washambuliaji wao kupenya safu ya ulinzi ya Twiga Stars inayoongozwa na Anastazia Katunzi, Noela Luhala na Ester Maseke, lakini ukuta huo uliokuwa imara na kucheza kwa umakini mkubwa uliowafanikisha kuzima mashambulizi yote na kufanya timu hizo ziende mapumziko kwa suluhu.

Kipindi cha pili kilianza Tanzania ilirudi kwa kasi na dakika 64 Opah Clement aliandikia bao Twiga Stars bao la kuongoza.

Bao hilo lilipunguza presha kwa Tanzania na kuwachanganya  wenyeji ambao walianza kucheza kwa presha kubwa wakisaka bao la kusawazisha. Hata hivyo, nidhamu ya mchezo na ustahimilivu wa wachezaji wa Twiga Stars uliwezesha timu hiyo kulinda ushindi huo muhimu hadi mwamuzi alipopuliza kipyenga cha mwisho kuashiria kumalizika kwa mchezo.

Matokeo haya yanawapa faida kubwa Tanzania kuelekea mchezo wa marudiano utakaopigwa Jumanne ya Oktoba 13, 2026, nchini Tanzania. Twiga Stars sasa inahitaji sare ya aina yoyote nyumbani ili kujihakikishia nafasi ya kusonga mbele katika hatua inayofuata ya mchujo huo wa Olimpiki.

Kama Twiga Stars itavuka hatua hiyo na kuiondoa Botswana katika mchezo wa marudiano, itatinga hatua ya tatu ambapo itakutana na mshindi wa kati ya Ethiopia na Rwanda, Ethiopia tayari ina faida ya bao 1-0 dhidi ya Rwanda.