Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tulia Ackson asisitiza kuinua soka la wanawake

TULIA Pict

Muktasari:

  • Tulia ambaye ni Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, amesema hayo leo Agosti 27, 2026 kwenye ufunguzi wa warsha ya siku tatu ya kuwajengea uwezo wasimamizi na viongozi wa soka la wanawake inayoendeshwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu la Kimataifa (FIFA) ikiandaliwa na TFF.

MJUMBE wa Bodi ya Wadhamini ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Dk Tulia Ackson, amesema uwekwe mpango mkakati wa soka la wanawake ili kuhakikisha mchezo huo unakua na kufikia viwango vya juu.

Tulia ambaye ni Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, amesema hayo leo Agosti 27, 2026 kwenye ufunguzi wa warsha ya siku tatu ya kuwajengea uwezo wasimamizi na viongozi wa soka la wanawake inayoendeshwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu la Kimataifa (FIFA) ikiandaliwa na TFF.

Amesema mafanikio ya wachezaji wa kike tayari yameifanya Tanzania kutambulika kwa kuwa na vipaji, hivyo viongozi wana wajibu wa kuweka mazingira yatakayowawezesha kufika mbali zaidi.

TULI 01

Pamoja na changamoto zilizopo, Tulia amesema Tanzania ipo katika hatua nzuri ya kusonga mbele, huku akisisitiza kuwa Bodi ya Wadhamini ya TFF iko tayari kushirikiana na viongozi na wadau kuhakikisha soka la wanawake linaendelea kupiga hatua.

Aidha, Tulia amewataka waliopewa dhamana ya kusimamia na kuendeleza soka la wanawake kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu, kuwapa moyo wachezaji na kutowakatisha tamaa wale wanaohitaji msaada wa kiufundi na kiuongozi.

“Tunataka kuwaona wachezaji wetu wakifika mbali zaidi na kuitangaza Tanzania kupitia vipaji vyao,” amesema Tulia.

TULI 02

Akizungumzia mchango wa Serikali, Tulia amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Samia Suluhu Hassan, ameendelea kutoa kipaumbele kwa maendeleo ya soka la wanawake pamoja na timu za vijana, akisisitiza kuwa hatua hiyo ni muhimu katika kujenga kizazi kipya cha wachezaji watakaoiwakilisha Tanzania kwa mafanikio.

Warsha hiyo ya siku tatu inalenga kuongeza maarifa na uwezo wa viongozi na wasimamizi katika kuendesha na kuendeleza soka la wanawake kwa mtazamo wa kimkakati na endelevu.