Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tshabalala atoa kauli nzito Yanga

New Content Item (1)


BEKI wa Yanga, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, amesema baada ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu uliopita, sasa kiu yao ni kuongeza mataji mengine ya ndani msimu huu huku wakielekeza nguvu kusaka ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika.


Akizungumza na Mwanaspoti, Tshabalala alisema imani hiyo inatokana na ubora wa kikosi walichonacho msimu huu, akieleza kuwa ushindani ndani ya timu ni mkubwa kutokana na uwepo wa wachezaji wenye viwango vya juu katika kila nafasi.

“Baada ya kuchukua ubingwa wa Ligi msimu uliopita, sasa tunatamani kuona tunachukua mataji yote ya ndani msimu huu. Tuna timu nzuri na ushindani ni mkubwa, hivyo tunaamini tuna uwezo wa kupigania kila taji,” alisema Tshabalala.

Tshabalala alisema kuwa, mafanikio ya ndani hayatoshi, kwani baada ya kuhakikisha wanatawala katika mashindano ya ndani, malengo yao yanaelekezwa pia kwenye medani ya kimataifa, hasa Ligi ya Mabingwa Afrika.

“Baada ya mataji ya ndani, tunatamani pia kufanya vizuri kimataifa na kubwa ni kuchukua ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika. Hilo ni jambo ambalo tunalitaka na tutapambana kulifikia,” alisema.

Aliongeza kuwa, mashabiki wa Yanga waendelee kuwa nyuma ya timu yao katika kipindi chote cha msimu, akisisitiza kuwa changamoto na presha zitakuwepo lakini hazipaswi kuwafanya kuyumba.

“Tunawaomba mashabiki wetu wawe nyuma ya timu, wasiyumbishwe na presha yoyote. Sisi wachezaji tunajua tunachotaka na tutaendelea kupambana kuhakikisha tunawapa furaha,” alisema Tshabalala.

Yanga imeanza msimu wa 2026-2027 vizuri kwa kubeba Ngao ya Jamii ikiifunga Simba bao 1-0, kisha ndani ya Ligi Kuu Bara imeshinda mechi zote sita ilizocheza na kukusanya pointi 18 ikikaa kileleni mwa msimamo kwa tofauti ya mabao dhidi ya Simba. Katika michezo hiyo, mabingwa hao wamefunga mabao 16 huku wakiruhusu mawili pekee.

Kimataifa, Yanga pia imeanza vizuri Ligi ya Mabingwa Afrika, baada ya kuitoa Gaborone United kwa jumla ya mabao 3-2. Ilianza kutoka sare ya 1-1 ugenini, kisha kushinda 2-1 nyumbani na kutinga hatua ya pili kuwania kufuzu makundi.

Tshabalala ambaye huu ni msimu wake wa pili ndani ya Yanga aliyojiunga nayo akitokea Simba alikodumu kwa takribani miaka 11, amekuwa na mchango wa bao moja alilofunga kwenye ligi dhidi ya Coastal Union.