Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

TPLB yapitisha bajeti ya Sh32 Bilioni kwa msimu wa 2026/27

Muktasari:

  • Kwa mujibu wa Mtunza Hazina wa TPLB, Ibrahim Mwayela, katika fungu hilo la fedha, kiasi cha Sh29 bilioni kitatumika katika kuendesha ligi.

Mkutano Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), leo Jumamosi, Novemba 14, 2026 umepitisha bajeti ya Sh32 bilioni kwa ajili ya msimu wa 2026/2027.

Kwa mujibu wa Mtunza Hazina wa TPLB, Ibrahim Mwayela, katika fungu hilo la fedha, kiasi cha Sh29 bilioni kitatumika katika kuendesha ligi.

Kiasi cha Sh1.5 bilioni kitatumika kwa ajili ya kugharamia watumishi wa Bodi ya Ligi Kuu.

Fedha takribani Sh1.4 bilioni zitatumika kwa ajili ya uendeshaji wa ofisi na fedha nyingine zitatumika kwa matumizi mengine.


MWENYEKITI DODOMA JIJI AULA

Katika hatua nyingine Mkutano Mkuu wa TPLB umempitisha Mwenyekiti wa Dodoma

Jiji FC, Joan Mazanda kuwa Mjumbe wa Bodi hiyo.

Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Kiomoni Kibamba amesema kuwa Mazanda amepitishwa kutokana na kuwa mgombea pekee baada ya mshindani wake Anita Rwezaula kutokidhi vigezo kikanuni.

"Anita Rwezaula alikuwa na ugomvi na kanuni za Uchaguzi na hivyo akaondolewa kwenye mchakato wa Uchaguzi na akabakia mgombea mmoja ambaye ni Joan Mazanda.

"Kanuni ya 19 kanuni ndogo ya nane ya kanuni za uchaguzi za TFF inafafanua kwamba kunapokuwa na mgombea mmoja, Mkutano Mkuu utamthibitisha mgombea huyo.

"Kwa mamlaka niliyopewa namtangaza Joan Mazanda kuwa Mjumbe wa Kamati ya Ligi Kuu," amesema Kibamba.