Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kiungo aziwazia Simba, Yanga

Muktasari:

  • Katika mahojiano yake aliyofanya Sudan, kiungo huyo alisema licha ya Singida kumuhitaji pia baada ya mkataba wake na Gor Mahia ya Kenya kuisha msimu wa 2025-2026, ila Simba ilionyesha uhitaji, kabla ya kushindwa kufikia makubaliano mazuri.

KIUNGO mshambuliaji wa Al-Merrikh SC ya Sudan, Mghana Enock Morrison amesema malengo yake siku moja ni kuchezea timu za Yanga au Simba, licha ya msimu wa 2025-2026, Singida Black Stars kuonyesha nia ya kumuhitaji na kushindwana mwishoni.

Katika mahojiano yake aliyofanya Sudan, kiungo huyo alisema licha ya Singida kumuhitaji pia baada ya mkataba wake na Gor Mahia ya Kenya kuisha msimu wa 2025-2026, ila Simba ilionyesha uhitaji, kabla ya kushindwa kufikia makubaliano mazuri.

Kiungo huyo alisema alikaribia kujiunga na Simba na alikuwa tayari kuichezea timu hiyo, ingawa walishindwa kukubaliana baadhi ya vipengele, jambo lililochangia pia kujiunga na Al-Merrikh SC ya Sudan, licha malengo yake ya kucheza Tanzania. “Yanga na Simba ni timu kubwa na nzuri kwa Ukanda wa Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla, hilo limejionyesha kutokana na wachezaji wakubwa kutoka mataifa mbalimbali wanaocheza, bado nina malengo ya kucheza siku moja,” alisema nyota huyo.

Nyota huyo aliyezaliwa Januari 18, 2000, ana uwezo wa kucheza kiungo wa kati kwa ufasaha, pia anauwezo wa kutokea pembeni. Amezichezea timu mbalimbali, zikiwamo za King Faisal FC na Asante Kotoko zote za kwao Ghana.

Kiungo huyo alishinda Tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya Kenya (MVP), baada ya kuiwezesha Gor Mahia kutwaa ubingwa wa 22, katika historia ya kikosi hicho maarufu ‘K’Ogalo.

Morrison alichangia mabao saba ya Gor Mahia msimu wa 2025-2026, kwa kufunga matatu na kuasisti manne katika mechi 31, alizocheza, alishinda Tuzo hiyo akiwa ni mchezaji wa kwanza wa kigeni kushinda baada ya miaka 14. Mara ya mwisho kwa mchezaji wa kigeni kushinda Tuzo ya (MVP), katika Ligi Kuu ya Kenya, alikuwa ni mshambuliaji raia wa Uganda, Dan Sserunkuma mwaka 2012, rekodi ambayo ilivunjwa na Morrison msimu wa 2025-2026, kutokana na kiwango kizuri.