Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tegis aitaka rekodi Afrika, aisubiri Tusker mapema

TEGIS Pict

Muktasari:

  • Nyota huyo aliyetua nchini msimu uliipita akiitumikia Pamba Jiji kwa mafanikio akiwa kwenye orodha ya nyota watatu wa idadi kubwa ya mabao (12) akizidiwa na aliyekuwa kinara Mossi Ndumumwe (17) na Feisal Salum aliyefunga 15.

STRAIKA wa Singida Black Stars, Mathew Tesigi amesema baada ya kuivusha timu hiyo hatua ya awali ya kombe la shirikisho Afrika, hesabu zake ni kusaka rekodi Afrika haswa ya kiatu cha mfungaji bora, huku akikiri kutoanza vyema Ligi Kuu.

Nyota huyo aliyetua nchini msimu uliipita akiitumikia Pamba Jiji kwa mafanikio akiwa kwenye orodha ya nyota watatu wa idadi kubwa ya mabao (12) akizidiwa na aliyekuwa kinara Mossi Ndumumwe (17) na Feisal Salum aliyefunga 15.

Msimu huu nyota huyo raia wa Kenya, ameanza vyema akiivusha SBS hatua ya awali ya kombe la shirikisho Afrika alipofunga mabao matatu ‘Hatitriki’ dhidi ya Al Ghazala Wau kwenye ushindi wa 7-1, mechi ya kwanza kisha kushinda 3-0 na kufuzu hatua inayofuata.

Singida Black Star inatarajia kukutana na Tusker FC ya nchini Kenya iliyoiondoka Al Ahli Wad Madani ya nchini Sudan, ambapo timu hizo zinatarajia kukutana katika hatua inayofuata ya kombe la shirikisho Afrika.

TEG 01

Tegis ameliambia Mwanaspoti kuwa baada ya kuanza vyema kwenye michuano hiyo, anasaka rekodi ya kiatu cha mfungaji bora ili kuandika historia mpya, akieleza kuwa lolote linawezekana kwakuwa anao uwezo.

Kuhusu kasi yake Ligi Kuu, amekiri kutoanza vyema akieleza kuwa vita ya namba dhidi ya mpinzani wake, Jonathan Sowah inampa wakati mgumu, lakini hata kukosa mechi tatu za mwanzo ilikuwa pigo kwake.

“Tusker nawajua kwakuwa nilishakutana nao nikiwa Shabana FC, japokuwa sikuwafunga ila nawahurumia tukikutana tena, kwa sasa hesabu zangu kwenye soka ni za juu, nawaza kuandika historia ya kiatu cha mfungaji bora Afrika.

TEG 02

“Ni kweli sijawa na makali Ligi Kuu ila ni mapema na sijakata tamaa, Singida BS ni timu kubwa yenye wachezaji wazoefu na wenye ubora, naamini nitarejea vyema na timu itafanya vizuri ukiacha matokeo tuliyoanza nayo,” amesema straika huyo.

Ametamba kuwa kutokana na ubora wa kikosi walichonacho na benchi la ufundi, SBS inaweza kufika fainali ya michuano hiyo Afrika, akieleza kuwa wamejipanga kufanya kweli kila mmoja kikosini.