Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

TDS yashusha mvua ya mabao, ikibeba ubingwa Dar Youth League

DAR Pict

Muktasari:

  • Mashindano hayo yalianza Mei 2026 na kufikia tamati leo katika Viwanja vya Ufundi, Lugalo, jijini Dar es Salaam ambapo kulikuwa na fainali nne.

TIMU ya vijana ya TDS chini ya miaka 18, imefanikiwa kuibuka bingwa wa mashindano ya Dar Youth League U-18 baada ya kuichapa Spotlight mabao 4-0, katika mechi ya fainali ya mwisho ya mashindano hayo kwa mwaka huu, ikiwa ni msimu wake wa saba.

Mashindano hayo yalianza Mei 2026 na kufikia tamati leo katika Viwanja vya Ufundi, Lugalo, jijini Dar es Salaam ambapo kulikuwa na fainali nne.

TDS, ambao huu ulikuwa msimu wao wa kwanza kushiriki michuano hiyo, ilimaliza hatua ya makundi ikiwa nafasi ya kwanza katika kundi A, kisha ikacheza nusu fainali dhidi ya Bulls FA na kushinda bao 1-0, kabla ya kukutana na Spotlight katika mechi ya fainali iliyoanza saa 10:00 jioni.

Akizungumza baada ya kumalizika kwa mashindano hayo, kocha wa TDS, Henry Sempa, alishauri kuwepo kwa mabadiliko katika mashindano ya wavulana wadogo. Alisema idadi ya wachezaji inatakiwa kuwa ndogo kuanzia wachezaji saba kila upande ili kuwasaidia kuongeza uwezo wa kuchezea mpira kwa muda mrefu wakiwa uwanjani, hali itakayowajenga zaidi kiwango chao.

Sempa, ambaye pia alikuwa na Timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 15 iliyoshiriki mashindano ya Kombe la Dunia nchini Azerbaijan, alisema wamefurahishwa sana na michuano ya Dar Youth League kwani inaongeza hali ya kujiamini na kuwafanya wachezaji waendelee kukomaa.

Naye Fadhil Said, miongoni mwa waandaji wa mashindano hayo, amesema: "Mwaka huu kwetu umekuwa wa mafanikio makubwa kwa sababu tumeongeza thamani ya mashindano. Ukiangalia kuna timu kama Simba na TDS ambazo zimeshiriki msimu huu, uwepo wao umeongeza kitu."

Fadhil pia aliwashukuru wadhamini wa mashindano hayo akisema: "Hakuna neno litakalotosha kuelezea shukrani zetu kwa wadhamini wetu Kisima, Golden, Howden. Kwa kiasi kikubwa wametushika mkono, na pia tunakaribisha makampuni mengine yanayotamani kuwa sehemu ya safari hii."