Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tanzania yashindwa kufuzu AFCON U-23 

Muktasari:

  • Mchezo huo wa dakika 90 nzito na zenye presha kubwa ulishuhudia vijana wa Tanzania wakipambana kufa na kupona kusaka ushindi wa tofauti ya mabao matatu, kufuatia matokeo ya mchezo wa kwanza ambapo Tanzania ilipoteza kwa mabao 4-1.

TIMU ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 23, Tanzania U-23 jioni ya leo imeondolewa katika  Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON U-23) licha ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Kenya katika mechi ya marudiano iliyopigwa kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Mchezo huo wa dakika 90 nzito na zenye presha kubwa ulishuhudia vijana wa Tanzania wakipambana kufa na kupona kusaka ushindi wa tofauti ya mabao matatu, kufuatia matokeo ya mchezo wa kwanza ambapo Tanzania ilipoteza kwa mabao 4-1.

Tangu dakika ya kwanza ya mchezo, Tanzania ilianza kwa kasi na kulishambulia lango la Kenya mfululizo, jitihada ambazo zilizaa matunda mapema baada ya Shekhan Khamis kufunga bao la pili kwa kichwa na kuamsha shangwe kwa mashabiki.

Ushindi huo wa mapema uliwaongezea kujiamini vijana wa Tanzania ambapo nyota Mwalimu alionyesha kiwango bora na kufunga bao la pili kwa penati.

Kipindi cha pili kilipoanza Selemani Mwalimu aliendelea kuibeba timu yake mgongoni baada ya kufunga bao lake la pili kwenye mchezo huo na kuifanya Tanzania kuongoza kwa mabao 3-0, matokeo ambayo kimahesabu yangeivusha moja kwa moja hadi hatua inayofuata.

Hata hivyo, mambo yalibadilika baada ya mshambuliaji wa Kenya, Andre Onyango kunufaika na makosa ya safu ya ulinzi ya Tanzania na kufunga bao pekee na la kufutia machozi la Kenya ambalo liliongeza wingi wa mabao na kubadilisha upepo wa mchezo huo kwa Tanzania.

Bao hilo la Onyango lilipoteza matumaini ya Tanzania kufuzu, kwani kulingana na hesabu za matokeo ya jumla, Tanzania ilihitaji ushindi usiopungua mabao 3-0 ili kuwaondoa wapinzani wao na kusonga mbele katika hatua za awali za michuano hiyo ambayo ingekutana na Ivory Coast katika mkondo wa pili.

Akizungumza na Mwanaspoti baada ya mechi kumalizika kiungo mshambuliaji wa Tanzania, Mohamed Shilla alisema: "Tulifanya makosa wenyewe na tumeambiwa lakini tumejifunza na tutapambana tena mashindano yajayo kuhakikisha tutafanya vizuri."
Kocha wa Tanzania, Ahmad Ally alisema: "Tumeshinda lakini hatujafuzu wachezaji walipambana lakini ndio hivyo mchezo wa mpira ni wa makosa."