Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba yaendelea kutembeza kipigo Ligi Kuu

Muktasari:

  • Mabao yote matatu ya mchezo huo yamepachikwa katika kipindi cha kwanza.

SIMBA imeendelea kutamba kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 leo Jumamosi, Novemba 21, 2026 katika Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Dar es Salaam.

Mabao yote matatu ya mchezo huo yamepachikwa katika kipindi cha kwanza.

JKT Tanzania ndio ilikuwa ya kwanza kupata bao kwenye mechi hiyo likipachikwa na Said Mkopi katika dakika ya 10.

Mkopi alifunga bao hilo kwa shuti kali la mguu wa kulia akimalizia pasi ya Hassan Kapalata.

Iliwachukua Simba dakika 10 tu kusawazisha bao hilo kupitia kwa Elie Mpanzu.

Mpanzu alifunga bao hilo katika dakika ya 20 akimalizia pasi ya Libasse Gueye

Dakika ya 34, Mpanzu naye alimpikia bao Libasse Gueye kwa pasi safi iliyomaliziwa kwa shuti la wastani na winga huyo raia wa Senegal.

Timu hizo zilienda mapumziko huku Simba ikiongoza kwa mabao 2-1.

Katika kipindi cha pili, JKT Tanzania na Simba zilishambuliana kwa zamu lakini hadi filimbi ya mwisho ilipopulizwa, Simba iliibuka kidedea.

Matokeo hayo yameifanya Simba iendelee kuongoza msimamo wa Ligi Kuu ya NBC ikifikisha pointi 33 katika mechi 11 ilizocheza hadi sasa.

JKT Tanzania imebaki katika nafasi ya tano ikiwa na pointi 17.

Hata hivyo, JKT Tanzania inaweza kushuka kwa nafasi moja iwapo Dodoma Jiji itaibuka na ushindi katika mecho iliyopangwa kuanza saa 3:00 usiku katika Uwanja wa Jamhuri Dodoma dhidi ya Fountain Gate.