Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tanzania Kabaddi hali tete India

KABADI Pict

Muktasari:

Katika mchezo uliotangulia, Tanzania ilipoteza dhidi ya Malaysia kwa pointi 43-26, kisha mchezo uliochezwa Oktoba 28, 2026, ilikubali kipigo cha pointi 35-28 kutoka Uganda.
 

TIMU ya Taifa ya Kabaddi ya Tanzania, imekubali kichapo cha pointi 48-20 dhidi ya India na kushindwa kufuzu nusu fainali ya mashindano ya Kabaddi ya Jumuiya ya Madola yanayofanyika nchini India.

Katika mchezo uliotangulia, Tanzania ilipoteza dhidi ya Malaysia kwa pointi 43-26, kisha mchezo uliochezwa Oktoba 28, 2026, ilikubali kipigo cha pointi 35-28 kutoka Uganda.

Hata hivyo, mchezaji Juma Sultan Nyingia kutoka Tanzania anaendelea kufanya vizuri, akiongoza orodha ya washambuliaji bora wa mashindano hayo ya jumuiya ya Madola.

Katika hatua ya makundi, Tanzania imecheza mechi tano kati ya hizo imeshinda moja dhidi ya England na kupoteza nne dhidi ya Malaysia, Sri Lanka, India na Uganda. Katika msimamo wa kundi A, Sri Lanka na wenyeji wa mashindano hayo, India zimetinga hatua ya nusu fainali baada kushinda mechi zote tano ilizocheza, huku kundi B, Kenya na Bangladeshi zikifuzu nusu fainali. Timu ya Nigeria haijafanikiwa kushinda mechi hata moja katika mashindano hayo na kupoteza bila kuwa na pointi ikiwa tofauti na England pamoja na Tanzania zilizoshinda mchezo mmoja mmoja na kupoteza nne.

Australia iliyopo kundi B, haina tofauti na Nigeria kwani haijapata ushindi badala yake imeishia kupoteza mechi nne ilizocheza.

Kwa wanawake, timu nne zilizofuzu nusu fainali ni Kenya  dhidi ya Uganda, huku India dhidi Sri Lanka, mechi zote zikitarajiwa kuchezwa leo Ijumaa.