Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Taifa Stars yabaki palepale viwango FIFA 

STARS Pict

Muktasari:

  • Kutocheza mechi za kirafiki za kalenda ya FIFA mwezi uliopita, kunaonekana kuchangia kwa kiasi kikubwa Taifa Stars kuganda katika nafasi ambayo ilikuwepo katika viwango vya awali.

TIMU ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' imebaki katika nafasi yake ya 112 kwenye viwango vya ubora vya Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) kwa mwezi Julai.

Kutocheza mechi za kirafiki za kalenda ya FIFA mwezi uliopita, kunaonekana kuchangia kwa kiasi kikubwa Taifa Stars kuganda katika nafasi ambayo ilikuwepo katika viwango vya awali.

Mabadiliko mengi ya nafasi yanaonekana kuchangiwa kwa kiasi kikubwa na Fainali za Kombe la Dunia zilizofikia tamati Jumapili iliyopita kwa Hispania kutwaa ubingwa.

Mabingwa hao wapya wa Kombe la Dunia, wamepanda kwa nafasi moja ambapo hivi sasa wanashika nafasi ya kwanza.

Kupoteza mechi ya fainali ya Kombe la Dunia dhidi ya Hispania kwa bao 1-0, kunaonekana kuigharimu Argentina ambayo imeanguka kwa nafasi moja kwenye viwango hivyo vya mwezi Julai, ikitoka nafasi ya kwanza hadi nafasi ya pili.

Matokeo ya mechi ya kuwania mshindi wa tatu katika Fainali za Kombe la Dunia ambayo yalikuwa ni ushindi wa mabao 6-4 wa England dhidi yaUfaransa yanaonekana kutobadilisha chochote katika viwango hivyo vya ubora vya FIFA kwa mwezi Julai.

Ufaransa ambayo imepoteza, bado imebakia katika nafasi yake ya tatu ya awali huku England ikibakia katika nafasi ya nne.

Norway inaonekana kunufaika kwa kiasi kikubwa na Fainali za Kombe la Dunia 2026 kwa vile ndio timu iliyopanda kwa nafasi nyingi zaidi kuliko nyingine.

Timu hiyo imepanda kwa nafasi 12 ambapo sasa ipo katika nafasi ya 19 kutoka nafai ya 31 ambayo ilikuwepo awali.