Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Taifa Stars ndo hivyo tena

STARS Pict

Muktasari:

  • Tanzania imefikisha pointi mbili baada ya sare mbili kwenye michezo minne lakini ikiwa tayari na tiketi ya kufuzu kama mwenyeji wa fainali hizo.

TIMU ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, itaendelea kusubiri kuona ushindi wake wa kwanza baada kulazimishwa sare isiyo na mabao nyumbani dhidi ya Nigeria, ikitengeneza ugumu wa nani atakwenda Fainali za Kombe la Mataifa Afrika 2027.

Kwenye mchezo huo uliopigwa Uwanja wa Amaan Zanzibar, licha ya Stars kutengeneza nafasi nyingi za kufunga kwenye kila kipindi, mashambulizi yao makali yaliishia kugonga miamba ambapo dakika ya 36 kipindi cha kwanza mshambuliaji Simon Msuva alitengeneza nafasi nzuri lakini shuti lake likagonga mwamba na kurudi mchezoni.

Kipindi cha pili, Stars ilitengeneza nafasi nyingine dakika ya 62 mshambuliaji Bernard Kamungo ambaye alipata nafasi ya kucheza mchezo wake wa kwanza kwenye kikosi hicho shuti lake la chini lilifanikiwa kumpita kipa wa Nigeria Stanley Nwabali na kugonga mwamba wa chini kisha mabeki kuokoa.

Nigeria itajutia nafasi kubwa walioyotengeneza dakika ya 90+2 baada ya kiungo wao Alex Iwobi kupiga krosi safi ambayo ilikosa mmaliziaji.

Matokeo hayo yanaipa kazi Nigeria kuhakikisha inatafuta ushindi katika mechi zilizosalia ili kupanda juu ya msimamo sasa ikiwa na pointi saba sawa na Guinea Bissau inayoongoza msimamo wa kundi hilo L, lakini Guinea jana ilikuwa inatarajiwa kuvaana na Madagascar ambapo kama imeshinda basi itakuwa imefikisha pointi kumi.

Tanzania imefikisha pointi mbili baada ya sare mbili kwenye michezo minne lakini ikiwa tayari na tiketi ya kufuzu kama mwenyeji wa fainali hizo.

Kundi hilo litanatakiwa kutoa timu moja pekee itakayofuzu fainali hizo ambapo sasa vita itakuwa kati ya Guinea na Nigeria ambazo zipo juu ya msimamo.


MATOKEO YA MECHI ZA KUFUZU AFCON 2027

Burundi 1-1 Zambia

Ethiopia 0-1 Msumbiji

Lesotho 2-1 Gabon

Malawi 0-0 Misri

Sudan Kusini 0-1 Angola

Tanzania 0-0 Nigeria