Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Stumai anahitaji msaada wa kisaikolojia

Muktasari:

  • Kwa kuwasaidia tu hapa kijiweni ni Stumai ametujulisha umma sababu inayomfanya asionekane uwanjani hivi sasa katika kikosi cha JKT Tanzania na Twiga Stars ni majeruhi yanayomkabili na sio ujauzito kama inavyovumishwa.

DADA yetu Stumai Abdallah juzi kati aliandika ujumbe mmoja wa kuhuzunisha sana katika ukurasa wake wa Instagram.

Kwa kuwasaidia tu hapa kijiweni ni Stumai ametujulisha umma sababu inayomfanya asionekane uwanjani hivi sasa katika kikosi cha JKT Tanzania na Twiga Stars ni majeruhi yanayomkabili na sio ujauzito kama inavyovumishwa.

Maana hadi amekanusha hana ujauzito basi lazima kuna mahali yatakuwa yamesemwa na ameyasikia au ameyaona yakiandikwa ndiyo akaamua kufunguka hali halisi.

Hapa kuna mambo mawili ya muhimu ambayo tunatakiwa tuyafanyie tafakuri ya kina katika lile andiko la straika wa mpira Stumai Abdallah.

Kwanza huyu mchezaji anaonekana majeraha yanayomkabili yanamuumiza sana kwa vile anakosa kuonekana uwanjani kwenye mechi za klabu yake na timu ya taifa.

Kwa mchezaji tena staa na tegemeo kama yeye, kukosa mechi ni jambo ambalo linaumiza. Linamnyima fursa ya kuendelea kuonyesha kipaji chake, pia kuna wakati anakosa baadhi ya stahiki kama posho na bonasi za mechi.

Jambo la pili ni hilo la kuzushiwa ana ujauzito. Hii sio sawa na kwa wanaofanya hivyo hawamtendei haki maana ni stori ya kutungwa ambayo haina uhusiano kabisa na changamoto inayomkabili.

Kwa wanaofanya hivyo wajue wanamuumiza sana kihisia Stumai na hiyo inaweza kusababisha pale atakapopona ashindwe kurudi katika makali yake.

Iko haja kwa Stumai kupata msaada wa kisaikolojia ili yanayoendelea mitandaoni dhidi yake yasimuathiri.