Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Masaka arejea baada ya siku 732

Muktasari:

  • Changamoto hiyo aliipata Novemba 8, 2024, wakati Masaka alipokuwa akicheza mchezo wake wa kwanza wa Ligi Kuu ya Wanawake England (WSL) akiwa na Brighton & Hove Albion Women dhidi ya Arsenal Women. Aliingia kipindi cha pili, lakini dakika chache baadaye akapata jeraha la bega lililomlazimu kutolewa kwa machela.

ZIMEPITA takribani siku 732, sawa na miaka miwili na siku mbili tangu mshambuliaji wa Tanzania, Aisha Masaka alipopata jeraha kubwa la bega katika mchezo dhidi ya Arsenal hadi kurejea mazoezini Novemba 10, 2026.

Changamoto hiyo aliipata Novemba 8, 2024, wakati Masaka alipokuwa akicheza mchezo wake wa kwanza wa Ligi Kuu ya Wanawake England (WSL) akiwa na Brighton & Hove Albion Women dhidi ya Arsenal Women. Aliingia kipindi cha pili, lakini dakika chache baadaye akapata jeraha la bega lililomlazimu kutolewa kwa machela.

Jeraha hilo lilikuwa pigo kubwa kwa mshambuliaji huyo ambaye alijiunga na Brighton akitokea BK Häcken ya Sweden Julai 2024, akiwa na matarajio ya kupata nafasi ya kuonyesha ubora wake kwenye moja ya ligi zenye ushindani mkubwa duniani.

Akizungumzia kipindi hicho kigumu, Masaka alielezea namna msimu wake wa kwanza Brighton ulivyokuwa mgumu, akieleza alikosa nafasi ya kucheza na kupata uzoefu aliouhitaji katika ligi hiyo.

Alisema: "Haikuwa msimu mzuri kwangu. Kwangu ni hatua kubwa kwa sababu WSL ni ligi kubwa duniani. Nahitaji uzoefu zaidi, nahitaji kucheza ili niweze kupata uzoefu huo."

Pamoja na hali hiyo, Masaka alieleza kipindi alichotumia akiwa nje kilimpa nafasi ya kujifunza kutoka kwa wachezaji wenye uzoefu, akiwataja Fran Kirby na Nikita Parris, ambao wamekuwa sehemu ya kikosi cha timu ya taifa ya wanawake ya England.

Alisema wachezaji hao walimsaidia kujifunza uvumilivu wakati wa kukabiliana na majeraha na kumtia moyo kuwa nafasi yake ya kufanya vizuri na kung'ara itafika.

Novemba 10, 2026, Masaka alirejea mazoezini, hatua inayoweza kuwa mwanzo wa kujenga wa safari yake baada ya kipindi kirefu cha kukabiliana na changamoto hizo.

Tangu ajiunge na timu hiyo msimu jana akitokea BK Hacken ya Sweden, nyota huyo alicheza mechi mbili kwa dakika 14 dhidi ya Arsenal (dakika 4) na Birmigham (dakika 10).