Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Straika Namungo haamini macho yake

LUKINDO Pict

Muktasari:

  • Kwa sasa amevuka idadi hiyo, jambo linaloonyesha maendeleo yake katika eneo la ushambuliaji na kuongeza matarajio ya kuendelea kufanya vizuri katika michezo iliyobaki ya msimu huu.

MSHAMBULIAJI wa Namungo FC, Herbert Lukindo amesema kiwango anachoonyesha katika Ligi Kuu Bara msimu wa 2026-2027 ni bora zaidi tangu aanze kucheza soka la ushindani, jambo linalompa hamasa ya kuendelea kupambana na kuweka rekodi mpya.

Akizungumza na Mwanaspoti, Lukindo amesema msimu huu umekuwa wa kipekee kwake baada ya kufikisha mabao sita, idadi ambayo hajawahi kuifikia tangu aanze kucheza Ligi Kuu Bara.

Amesema mafanikio hayo yamemjengea imani anaweza kufanya makubwa zaidi, huku akitaja ushirikiano na wachezaji wenzake pamoja na kufuata maelekezo ya kocha ni miongoni mwa sababu za kiwango chake.

“Katika kariba yangu sijawahi kufikisha idadi kubwa ya mabao kama sasa. Hii inanipa motisha ya kuamini kila kitu chini ya jua kinawezekana. Siri ya kiwango hiki ni ushirikiano na wenzangu na kufuata maelekezo ya kocha mkuu,” amesema Lukindo.

Mshambuliaji huyo alianza safari yake ya soka jijini Tanga katika kituo cha Eagle Rangers Sport Academy, kabla ya kuendelea kuzitumikia JKT Mgambo, Ndanda FC, Mbao FC, Mbeya City, Pamba Jiji, Biashara United na KenGold FC.

Amesema ataendelea kupambana na kuitumikia Namungo kwa uwezo wake wote kila anapopata nafasi ya kucheza. Mabao sita aliyofunga msimu huu yanamfanya kuwa sawa na Maabad Maulid wa Coastal Union katika orodha ya wafungaji. Hata hivyo, wanazidiwa na Anuary Jabir wa Polisi Tanzania na Peter Shalulile wa Yanga, ambao kila mmoja amefunga mabao saba.

Kabla ya kujiunga na Namungo FC Agosti 21, 2025, akitokea KenGold FC, Lukindo alikuwa ameonyesha pia kiwango kizuri katika msimu wa 2024-2025, alipofanikiwa kuifungia timu hiyo mabao manne ya Ligi Kuu Bara.

Kwa sasa amevuka idadi hiyo, jambo linaloonyesha maendeleo yake katika eneo la ushambuliaji na kuongeza matarajio ya kuendelea kufanya vizuri katika michezo iliyobaki ya msimu huu.