Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Starkie aanza kibabe England

STAR Pict
STAR Pict

Muktasari:

  • Starkie, ambaye alipitia kipindi kigumu msimu uliopita kutokana na majeraha yaliyomweka nje ya uwanja kwa msimu mzima hivi sasa ameonekana kurejea kwenye kiwango chake na kuanza kuwavutia mashabiki wa klabu hiyo.

KIUNGO mshambuliaji wa Tanzania, Ben Starkie anayekipiga Truro City FC inayoshiriki Ligi Daraja la Sita England (National League South) ameanza na mguu mzuri kwenye kikosi cha timu hiyo hiyo baada ya msimu jana kukaa nje msimu mzima.

Starkie, ambaye alipitia kipindi kigumu msimu uliopita kutokana na majeraha yaliyomweka nje ya uwanja kwa msimu mzima hivi sasa ameonekana kurejea kwenye kiwango chake na kuanza kuwavutia mashabiki wa klabu hiyo.

Hadi sasa, nyota huyo wa Mtanzania tayari ameitumikia Truro City jumla ya mechi 10 katika ligi msimu huu, huku akionyesha mchango mkubwa kwenye safu ya ushambuliaji.

Alionyesha ubora zaidi alipopachika bao lake la kwanza la msimu katika mchezo wa Kombe la FA (Emirates FA Cup) dhidi ya Merthyr Town FC.

Katika pambano hilo, Starkie alisaidia timu hiyo kuibuka na ushindi mnono wa mabao 2-0, matokeo yaliyowawezesha kutinga hatua inayofuata ya mashindano hayo kongwe England.

Urejeo wa Starkie si tu kwamba yanawapa matumaini mashabiki wa Truro City, bali pia yanatoa picha nzuri kwa benchi la ufundi la Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ chini ya kocha Miguel Gamondi kuelekea mechi zijazo za kufuzu AFCON, ikizingatiwa kuwa kiungo huyo amekuwa miongoni mwa vijana wenye vipaji vikubwa wanaoitangaza nchi Ulaya.