Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

SIRI KUBWA YANGA!

Kocha wa Yanga Sam Timbe.

SIRI KUBWA YANGA! MWANDISHI WETU SIRI ya kitaalamu ya kufanya vibaya kwa Yanga katika mechi za mwanzo za Ligi Kuu Tanzania Bara imefahamika. Kocha wa Al Hilal ya Sudan, Sredojevic Milutin Micho anaamini kuwa timu hufanya kazi kama binadamu na kwamba timu ina uti wa mgongo kama ilivyo kwa binadamu. Anasema kuwa kunapotokea kwa tatizo katika uti wa mgongo, binadamu hawezi kufanya kazi na pia uti wa mgongo wa timu unapovunjika, timu hufanya vibaya uwanjani. Micho alifafanua kuwa uti wa mgongo wa timu unaundwa na kipa (namba 1), beki wa kati (namba 5), viungo wawili wa kati (namba 6 na 8) na mshambuliaji (namba 9). "Hata ukiwapanga uwanjani utaona wamefuatana na kuunda mstari moja. Mbele ya kipa kuna sentahafu, mbele kuna viungo namba sita na nane na mbele ya kuna namba tisa. Ndio maana unaitwa uti wa mgongo," anafafanua. Micho alisema wachezaji hao watano, lazima wawe fiti ili timu ishinde, na iwapo itatokea wachezaji watatu katika namba hizo wakawa majeruhi, basi timu huwa inayumba. Na hiyo ndio siri ambayo imeifanya Yanga kusuasua katika mechi za mwanzo za Ligi Kuu kutokana na wachezaji wanaounda uti wa mgongo kuwa majeruhi karibu wote ukiondoa viungo wa kati wawili; Juma Seif Kijiko na Haruna Niyonzima 'Fabregas' ambao ndio wapo fiti. Kipa Yaw Berko ni majeruhi, sentahafu Nadir Haroub Cannavaro ni majeruhi kama ilivyo kwa sentafowadi; Davies Mwape, Kenneth Asamoah na Jerry Tegete ambao wote ni majeruhi. Taaluma ya ukocha inaonyesha kuwa timu bora na inayotamba uwanjani, ni lazima iwe na wachezaji hao watano imara uwanjani, ingawa wachezaji wanaocheza nafasi nyingine nao ni muhimu pia, lakini hao watano ndio nguzo ya timu. Lakini wakati Yanga ikiwa na tatizo hilo, Micho pia amewahi kuichambua alipoifunga mabao 6-2 katika mechi mbili mjini Khartoum mwezi huu kuwa timu hiyo ya Jangwani ilikuwa na tatizo la kutotafuta ushindi kwa kupiga pasi za mbele, badala yake wamekuwa wakipiga pasi nyingi za pembeni (square pass). Yanga ilifungwa na JKT Ruvu bao 1-0 kabla ya kutoka sare ya 1-1 na Moro United katika mechi za nyumbani kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro jambo ambalo limewatia hasira mashabiki wa timu hiyo ya Jangwani. Hata hivyo, uti huo wa mgongo wa Yanga unatarajiwa kuwa imara baada ya wachezaji hao kuanza kurejea moja baada ya mwingine kwani wengi wao wamepata nafuu na wataanza kuonekana katika mchezo ujao wa Ligi Kuu Bara.