Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Singida yamfuata Mgaboni

Muktasari:

  • Mwanaspoti linafahamu kuwa Uongozi wa klabu hiyo umevutiwa na uwezo wa mshambuliaji huyo na unaamini anaweza kuongeza makali kwenye safu ya ushambuliaji ambayo inatarajiwa kufanyiwa maboresho makubwa kabla ya kuanza kwa msimu huo.

SINGIDA Black Stars imeanza harakati za kuinasa saini ya mshambuliaji raia wa Gabon, Nathanael Ndwangou, ikiwa ni sehemu ya maboresho ya kikosi kuelekea msimu wa mashindano 2026-2027.

Mwanaspoti linafahamu kuwa Uongozi wa klabu hiyo umevutiwa na uwezo wa mshambuliaji huyo na unaamini anaweza kuongeza makali kwenye safu ya ushambuliaji ambayo inatarajiwa kufanyiwa maboresho makubwa kabla ya kuanza kwa msimu huo.

Mpaka sasa mazungumzo kati ya pande hizo yanaendelea, huku klabu hiyo ikisaka makubaliano yatakayomuwezesha Ndwangou kutua nchini na kujiunga na kikosi hicho katika dirisha hili la usajili.

Taarifa za ndani kutoka kwenye klabu hiyo zilisema viongozi wana matumaini ya kukamilisha dili hilo mapema ili kumpa kocha muda wa kutosha kumjumuisha mchezaji huyo katika maandalizi ya msimu mpya.

“Ni mchezaji ambaye amependekezwa kutokana na ubora wake katika eneo la ushambuliaji. Mazungumzo yanaendelea vizuri na kila upande unaonyesha nia ya kufikia makubaliano,” zilidai taarifa hizo.

“Kuhusu wingi wa wachezaji wapo ambao watatolewa kwa mkopo ili kukamilisha idadi kamili inayotakiwa kwa mujibu wa sheria.” 

Singida imekuwa miongoni mwa timu zinazofanya maboresho makubwa ya kikosi katika kipindi hiki cha usajili, huku ikiongoza kwa kuwa na wachezaji wengi wakigeni kuliko idadi inayotakiwa (12).

Iwapo usajili huo utakamilika, Ndwangou atakuwa mmoja wa nyota wapya wanaotarajiwa kuongeza nguvu katika safu ya ushambuliaji ya Singida Black Stars, huku mtihani ukiwa kwa kocha kwenye hesabu za kusuka nani abaki na yupi atolewe kwa mkopo.