Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Singida BS yamrejesha Kyombo

Muktasari:

  • Mshambuliaji huyo aliyewahi kuitumikia Singida kabla ya kuamua kutafuta changamoto sehemu nyingine, amerejea ndani ya kikosi hicho baada ya kuachana na Polisi Tanzania, aliyojiunga nayo Julai 30, 2026, akitokea NAPSA Stars ya Zambia.

UONGOZI wa Singida Black Stars umefikia makubaliano ya kumrejesha aliyekuwa mshambuliaji wa timu hiyo, Habib Kyombo ili kuongeza nguvu eneo hilo la ushambuliaji, japo ataanza kukichezea kikosi hicho katika dirisha dogo la Januari 2027.

Mshambuliaji huyo aliyewahi kuitumikia Singida kabla ya kuamua kutafuta changamoto sehemu nyingine, amerejea ndani ya kikosi hicho baada ya kuachana na Polisi Tanzania, aliyojiunga nayo Julai 30, 2026, akitokea NAPSA Stars ya Zambia.

Nyota huyo alijiunga na NAPSA Stars ya Zambia, Aprili 10, 2026, akiwa mchezaji huru baada ya kuachana na Mbeya City, kisha msimu wa 2026-2027, akarejea Bongo na kusaini Polisi Tanzania ambayo ameachana nayo.

Kyombo aliwahi kucheza Singida kwa nyakati tofauti. Pia amezitumikia Mbao, Simba, Pamba Jiji na Mamelodi Sundowns FC ya Afrika Kusini.

Nyota huyo amefikia uamuzi wa kuachana na Polisi Tanzania kwa makubaliano ya pande mbili, huku akiwa ameifungia timu hiyo bao moja msimu wa 2026-2027 katika Ligi Kuu waliposhinda 2-0 dhidi ya JKT Tanzania, Agosti 20, 2026

Mechi hiyo iliyochezwa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha, Kyombo alifunga bao hilo dakika ya 65, baada ya Kenny Ally Mwambungu kuitangulizia Polisi Tanzania dakika ya 45.

Usajili huo ni wa pili kwa Singida inayofundishwa na Kocha Mkuu, Mkongomani Papy Kimoto kuelekea dirisha dogo la Januari 2027, baada ya kumtambulisha aliyekuwa winga wa Simba, Luis Miquissone aliyeachana na Al-Ahly Benghazi SC ya Libya.