Simba, Yanga zamkosa Mhabeshi
Muktasari:
- Wakuma amekuwa akihusishwa na Simba Queens katika dirisha hili la usajili baada ya kiwango bora alichoonyesha msimu uliopita, ambapo aliisaidia CBE kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake Ethiopia na kufuzu kucheza Ligi ya Mabingwa Afrika kupitia michuano ya CECAFA.
LICHA ya mkataba wa mshambuliaji wa kimataifa wa Ethiopia, Senaf Wakuma, kumalizika mwishoni mwa Juni mwaka huu, inaonekana Simba Queens na Yanga Princess huenda zikashindwa kumpata nyota huyo baada ya klabu yake Commercial Bank of Ethiopia (CBE Women) kuonyesha nia ya kuendelea naye.
Wakuma amekuwa akihusishwa na Simba Queens katika dirisha hili la usajili baada ya kiwango bora alichoonyesha msimu uliopita, ambapo aliisaidia CBE kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake Ethiopia na kufuzu kucheza Ligi ya Mabingwa Afrika kupitia michuano ya CECAFA.
Hata hivyo, taarifa kutoka Ethiopia zinaeleza kuwa CBE imeanza mazungumzo ya kumbakiza mshambuliaji huyo kutokana na umuhimu wake ndani ya kikosi.
Uongozi wa klabu hiyo unaamini Wakuma bado ana mchango mkubwa katika malengo yao ya kutetea ubingwa wa ligi na kufanya vizuri kwenye mashindano ya kimataifa.
Iwapo mazungumzo hayo yatafanikiwa, itakuwa pigo kwa Simba Queens ambao wamekuwa wakitafuta mshambuliaji mwenye uwezo mkubwa wa kufunga mabao ili kuimarisha safu yao ya ushambuliaji kuelekea msimu mpya.
Simba wanahitaji huduma yake ili kuziba nafasi ya Jentrix Shikangwa ambaye alitimka kikosini hapo baada ya kupata ofa kubwa kutoka FC Masar ya Misri.
Yanga Princess pia ilivutiwa na huduma ya nyota huyo, hasa baada ya kufanikiwa kumsajili aliyekuwa kiungo wa CBE, Aregash Kalsa.
“Ndio timu za Tanzania zilikuwa zinamuhitaji hasa Simba lakini C.B.E wako kwenye mazungumzo naye ya kuendelea kumbakiza.