Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mambo matatu usajili wa kiungo Yanga

USAJILI Pict


INAONEKANA kiungo wa zamani wa Shamakhi FC ya Ligi Kuu Azerbaijan, Alphonce Mabula ameanza kuvutiwa na mpango wa Yanga baada ya klabu hiyo kumuwekea mezani baadhi ya vigezo vinavyoweza kumbadilisha mawazo na huenda msimu ujao wa 2026-2027 akacheza Ligi Kuu ya NBC.


Kuna mambo matatu juu ya dili hilo na taarifa ambazo Mwanaspoti limezipata zinaeleza pamoja na Yanga kuendelea na mazungumzo ya ofa, imemuahidi kumpatia jezi namba nane kama watafikia makubaliano, jezi ambayo kwa wananchi anaitumia Lassine Kouma ambaye huenda akatimka kikosini hapo.


Inaelezwa jezi namba nane aliyokuwa akiitumia Mabula msimu wake wa pili akiwa na Shamakhi FC ina historia kubwa kwenye maisha yake kisoka.

Mbali na jezi hiyo, jambo la pili lililitajwa kumuhusu kiungo huyo mkabaji ni ukaribu wake na baadhi ya marafiki wengi alionao Bongo ikielezwa kuwa umeanza kumshawishi kuangalia kwa jicho la pili uwezekano wa kurejea nyumbani baada ya miaka kadhaa ya kucheza soka la kulipwa nje ya nchi.

MABU 02

Hata hivyo, mazungumzo bado yanaendelea kwani jambo la tatu linaloonekana kuwa la msingi zaidi ni kwamba Yanga haijafikia dau la Sh1.5 bilioni, kiasi ambacho Wananchi wanapaswa kukitoa ili kukamilisha dili hilo.

Wakati Yanga ikiendelea kumshawishi Mabula, pia kiungo huyo inatajwa kuwa ana ofa kutoka Kasımpasa S.K ya Ligi Kuu Uturuki ambayo imeambiwa ili kumpata inapaswa kutoa kiasi cha Sh2 bilioni ili kuinasa saini yake.

“Ni kweli Yanga inapambana kukamilisha dili hilo na hadi sasa bado mambo hayajakaa sawa, mwanzoni alipotafutwa mchezaji alikuwa hajavutiwa na kurudi kucheza Ligi ya Tanzania, lakini kwa sasa ni kama amelainishwa, nafikiri tusubiri kuona,” kilisema chanzo hicho.

MABU 01

Mwanaspoti iliwahi kufanya mazungumzo na Mabula kuhusu uwezekano wa kurejea kucheza Tanzania na kiungo huyo aliweka wazi kuwa kwa kipindi hicho kipaumbele chake kilikuwa ni kuendelea kucheza nje ya nchi ili kupata masilahi mazuri zaidi na kuongeza uzoefu katika maisha yake ya soka.

“Naangalia kazi yangu na lazima pesa iwepo. Malengo yangu ni kuendelea kucheza Ulaya,” aliwahi kusema Mabula wakati alipomaliza mkataba wake na Shamakhi Juni 30, 2026.

Katika misimu miwili aliyocheza Shamakhi FC, Mabula alionesha ubora wake kwa kucheza mechi 45 za Ligi Kuu Azerbaijan, akifunga mabao matano na kutoa pasi 12 za mabao. Msimu wa 2025-2026 alicheza mechi 28, akifunga mabao mawili na kutoa pasi tisa za mabao.

MABU 03

Kabla ya kutua Shamakhi Januari 2025 akiwa mchezaji huru, alikuwa mchezaji wa Spartak Subotica ya Serbia aliyoanza kuitumikia Februari 2022, alipojiunga nayo akitokea kikosi cha Alliance FC. Pia amecheza RFK Novi Sad msimu wa 2024-2025 kwa mkopo.

Kwenye kikosi cha Timu ya Taifa, Taifa Stars, Mabula aliitwa kwa mara ya kwanza Mei 30, 2025 chini ya kocha Hemed Suleiman ‘Morocco’ kwa mchezo wa kirafiki dhidi ya Afrika Kusini na mashindano ya COSAFA dhidi ya Eswatini na Madagascar.

Tangu hapo nyota huyo mwenye umri wa miaka 23, ameendelea kuitwa Taifa Stars na kucheza kwa kiwango kikubwa kiasi cha kuvutia klabu mbalimbali.