Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba yaanza na gia kubwa, kuweka kambi Arusha

BAADA ya kurejea nchini, mabosi wazito wa Simba walikutana faragha jijini Dar es Salaam kupanga mikakati mipya ya namna kuanza msimu kwa kishindo wakiwa kwenye ubora wao uliozoeleka.

Simba walikuwa kambini nchini Morocco kama ilivyokuwa kwa watani wao wa jadi, kujiweka sawa kwa Ligi Kuu Bara na michuano ya kimataifa.

Mwanaspoti ilishuhudia jana mabosi hao wakiingia kwenye kikao hicho kizito, licha ya kufanya siri kubwa lakini habari zinasema kwamba ajenda kubwa ilikuwa Simba Day pamoja na kambi mpya ya kujiandaa.

Habari zinasema kwamba Simba Day itafanyika Septemba 19 kama ilivyopangwa kwenye Uwanja wa Mkapa lakini bado mpaka jana jioni walikuwa hawajakubaliana ni timu gani ije na mezani tayari walikuwa nazo tatu ikiwemo moja ya Uarabuni.

“Kambi tutaweka kule Karatu, Arusha kukamilisha maandalizi ya mwisho mwisho kujiweka sawa,” alidokeza kiongozi mmoja licha ya kukiri kwamba kuna wengine walitaka kambi hiyo iende Zanzibar ambako wamekuwa wakiweka na kupata mafanikio kwenye miaka ya hivi karibuni.

Simba imepania kuhakikisha kwamba kikosi chake kinakaa sawa kabla ya mechi ya Simba Day na wafanye makubwa kuliko Siku ya Mwananchi ambayo Yanga waliiadhimisha juzi Jumapili na kujaza Uwanja wa Mkapa.

Simba imekuwa na utamaduni wa kufanya vizuri kwenye siku hiyo kutokana na mpangilio wao na staili zao za utambulishaji wa wachezaji ingawa msimu huu watamkosa msemaji wao, Haji Manara ambaye amevuka boda akatua Yanga. Simba ambayo haijafanya mabadiliko makubwa kwenye kikosi chake, Kocha wao Didier Gomes amesisitiza kwamba lengo lao kimataifa msimu ujao ni kutinga nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.