Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba wavunja mkataba wa Mhilu Kagera

Baada ya kuwepo sintofahamu kuhusu usajili wa mshambuliaji nyota wa Kitanzania, Yusf Mhilu hatimaye klabu yake imetoa baraka kwa mchezaji huyo.

Mhilu alitambulishwa Simba Agosti 4 mwaka huu kuwa mchezaji wao huku uongozi wa Kagera ukisema hawajamalizana na mchezaji huyo kwakuwa wana mkataba nae.

Leo kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram wameandika; "Tumefikia makubaliano ya pande zote mbili (Kagera Sugar FC na Simba Sc) juu ya uhamisho wa aliyekuwa mchezaji wetu Nyota Yusuph Valentine Mhilu kwa dau la Sh40 milioni.

Wameendelea kuandika; "Mhilu alisaini kandarasi ya miaka miwili kuitumikia Kagera Sugar mwaka jana 2020. Hivyo uhamisho huu wa kwenda Simba ni uhamisho ambao umehusisha kuvunja mkataba wake wa mwaka mmoja uliosalia ndani ya klabu ya Kagera Sugar,"

Mhilu alikuwa miongoni mwa wachezaji wa kikosi cha Msimbazi walioenda kwenye kambi ya maandalizi ya msimu mpya nchini Morocco