Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba ya moto, Rushine aipa jeuri

KWARAA Pict

Muktasari:

  • Bao la dakika ya 33 kipindi cha kwanza likifungwa na beki na nahodha msaidizi wa kikosi hicho, Rushine De Reuck, likatosha kuihakikishia Simba ushindi huo, akifunga kwa kichwa wakati akitumia mpira wa adhabu ndogo iliyopigwa na Nathaniel Chilambo.

SIMBA imeendelea kuwa ya moto baada ya kushinda mchezo wake wake wa tisa mfululizo msimu huu ikizidi kujikita juu ya msimamo wa Ligi Kuu Bara, ikiwa timu pekee ambayo haijapoteza mchezo wowote, ikiichapa Fountain Gate kwa bao 1-0.

Bao la dakika ya 33 kipindi cha kwanza likifungwa na beki na nahodha msaidizi wa kikosi hicho, Rushine De Reuck, likatosha kuihakikishia Simba ushindi huo, akifunga kwa kichwa wakati akitumia mpira wa adhabu ndogo iliyopigwa na Nathaniel Chilambo.

Ushindi huo unaifanya Simba kufikisha pointi 27 ikiendelea kuwa juu ya msimamo wa ligi ikiwaangalia kwa chini Yanga waliopo nafasi ya pili na pointi zao 22.

KWAR 02

Wakati bao hilo likifungwa, ilimlazimu mwamuzi Raphael Ikambi kurudi kwenye marudio ya FVS kujiridhisha ikionekana kuwa kama mfungaji alikuwa ameotea na kuamua iwe bao, hata hivyo wenyeji wakiongozwa na kocha wao, Fred Felix Minziro walionekana kulalamikia bao hilo.

Simba ndio timu iliyokuwa imetengeneza nafasi nyingi za kufunga ambapo mpaka mapumziko ilikuwa imepiga mashuti matano yaliyolenga lango na moja likawa bao huku Fountain wakiwa hawajapiga shuti lolote.


KWAR 03

FOUNTAIN KIPA YUPO
Fountain ingeweza kupoteza vibaya mchezo huo kama isingekuwa ubora wa kipa Machupa Kapili ambaye alikuwa na mchezo bora akiizuia Simba kwenye mashambulizi saba ya wazi akionyesha uwezo bora langoni.


NAFASI KUBWA FOUNTAIN
Fountain nafasi yao bora zaidi ilitengenezwa dakika ya 63 ya kipindi cha pili, Ramadhan Seif anashindwa kumalizia kazi nzuri iliyofanywa na Saddick Ramadhan akishindwa kumaliza krosi nzuri ikiwa ndefu kwake.


KWAR 01

FOUNTAIN WAKO FITI
Kama kuna kitu kiliwapa Simba wakati mgumu kwwenye mchezo huo ni namna wenyeji wao Fountain Gate walivyokuwa fiti ambapo walionekana kuwa Daraja moja la utimamu wa mwili na wakundu hao na kufanya makosa kuwa machache uwanjani.


SIMBA MECHI 34 BILA KUPOTEZA
Kama unahesabu ni kwamba Simba imeendelea kuwa moto ikicheza mechi 34 bila kupoteza ambapo kati ya hizo imeshinda 28 na kutoa sare sita , mara ya mwisho kwa wekundu hao kupoteza kwenye ligi ilikuwa Desemba 7, 2025 ilipochapwa mabao 2-0 dhidi ya Azam FC.