Makundi CAF msiende na matokeo
Muktasari:
- Ilikuwa lazima tufuatilie kwa umakini maana timu zetu nne zinashiriki mashindano hayo na zote zimeingia katika hatua ya makundi ambayo ni mwanzo wa zile hatua dume za mashindano hayo.
JANA tulikuwa bize hapa kijiweni kufuatilia tukio la kupanga makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho Afrika msimu huu.
Ilikuwa lazima tufuatilie kwa umakini maana timu zetu nne zinashiriki mashindano hayo na zote zimeingia katika hatua ya makundi ambayo ni mwanzo wa zile hatua dume za mashindano hayo.
Simba ikapangwa na Berkane, Orlando Pirates na timu inaitwa Colombe sijui huku Yanga ikipangwa na Zamalek, MC Alger na Club Africain.
Azam imepangwa na FAR Rabat, Durban City na Al Ahli Tripoli huku Singida Black Stars ikikutanishwa na Maniema, Belouizdad na
Sasa tutoe tahadhari mapema maana baada tu ya makundi kupangwa, tumeona mashabiki, wanachama, maofisa na baadhi ya viongozi wa timu zetu wakianza kutamba lazima watoboe kwenda robo fainali.
Lakini kutamba kwao ni kule ambako kumepitiliza maana hawatoi hata nafasi ndogo ya kuheshimu wapinzani ambao wamepangwa nao ila wanaamini wao ndio wababe wa makundi hayo.
Kiuhalisia hakuna timu iliyo rahisi kwenye hatua hiyo tofauti na baadhi yetu wanavyoaminishana mitaani na kwenye mitandao ya kijamii timu zetu zitatesa kwenye makundi.
Hili likifahamika itasaidia watu kutokuwa na matokeo yao mfukoni kama wanavyoanza kuyaweka hivi sasa na hivyo mechi za makundi zikianza, angalau itasaidia kupunguza matarajio makubwa yanayowekwa na timu zetu.
Tukumbuke wakati sisi tunajiandaa na wenzetu pia wanajiandaa hivyo hatutakiwi kujimaliza sana kabla hatua ya makundi haichezwa hata raundi moja.