Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba kuja na sapraizi juni 25

SIMBA Pict

Muktasari:

  • Awali Wekundu hao walikuwa na mzuka mwingi wa kutaka ngoma hiyo ipigwe Juni 15 kama ilivyopangwa upya na Bodi ya Ligi baada ya kuahirishwa Machi 8, licha ya Yanga kutoa msimamo wa kuigomea mechi hiyo iliyotarajiwa kupigwa jana, kabla ya Ijumaa iliyopita walikatwa stimu baada ya kupangwa tarehe mpya baada ya kikao kizito cha mabosi wa klabu hizo walioitwa Ikulu Dodoma.

HAKUNA ubishi huko mtaani na mtandaoni mashabiki na wapenzi wa Simba bado hawana furaha  kutokana na kitendo cha Dabi ya Kariakoo kuahirishwa kutoka jana Jumapili hadi Juni 25, lakini kuna kitu kama kitafanya na timu hiyo badi itawasapraizi wengi katika ishu ya ubingwa wa Ligi Kuu Bara.

Awali Wekundu hao walikuwa na mzuka mwingi wa kutaka ngoma hiyo ipigwe Juni 15 kama ilivyopangwa upya na Bodi ya Ligi baada ya kuahirishwa Machi 8, licha ya Yanga kutoa msimamo wa kuigomea mechi hiyo iliyotarajiwa kupigwa jana, kabla ya Ijumaa iliyopita walikatwa stimu baada ya kupangwa tarehe mpya baada ya kikao kizito cha mabosi wa klabu hizo walioitwa Ikulu Dodoma.

Vigogo hao wa Simba na Yanga waliitwa Ikulu y Chamwino na kuzungumza na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kabla ya kutolewa tarehe mpya ya Dabi na sasa itapigwa Juni 25 Kwa Mkapa na kumaliza sintofahamu iliyojitokeza, huku upande wa Yanga ukionekana kufurahia zaidi.

Hata hivyo, kuna kitu ambacho baadhi ya wadau wanaamini huenda Simba ikawasapraizi katika mechi hiyo ya kuamua bingwa wa msimu huu kama ilivyowahi kutokea katika msimu wa 2016-2017 wakati Yanga ilipobeba ubingwa ‘jioni’ bila kutarajiwa siku ya kufungwa kwa msimu huo ikiiduwaza Simba.

Ipo hivi. Mechi hiyo ya Dabi ya Kariakoo iliyopangwa kupigwa Juni 25 kuanzia saa 11:00 jioni kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam ndio ulioshikilia hatma ya ubingwa wa Ligi Kuu Bara kwa msimu huu kama ilivyokuwa katika msimu huo wa 2016-2017.

Kabla ya kukutana katika mechi hiyo itakayokuwa ya 114 kwa timu hizo katika Ligi ya Bara tangu ilipoasisiwa 1965, kila moja itacheza michezo miwili, Simba ikitarajiwa kuvaana na timu zilizoshuka daraja mapema, KenGold na Kagera Sugar wakati Yanga ikacheza na TZ Prisons na Dodoma Jiji.

Yanga kwa sasa inaongoza msimamo wa Ligi ikiwa na pointi 73, moja zaidi na ilizonazo Simba yenye 72 ikishika nafasi ya pili kila moja ikiwa imecheza mechi 28 na kwa maana hiyo kila moja ikishinda mechi hizo mbili zitavuna alama sita na kuongeza hazina walizonazo.

Kama Yanga itazifunga Prisons na Dodoma Jiji itafikisha jumla ya pointi 78, wakati kwa Simba ikipeta mbele ya KenGold na Kagera ikavuna jumla ya pointi 78 ndipo Juni 25 zitaenda kuvaana huku Kombe likiwa uwanjani na timu yoyote itakayoshinda basi itakuwa bingwa na kupewa taji siku hiyo.

Baadhi ya wadau wa soka wanaamini Simba ina nafasi kubwa ya kuiduwaza Yanga kama ilivyofanya kwa kupunguza pengo la pointi kutoka 13 hadi kubakiza moja, tofauti na ilivyokuwa ikifikiriwa mwanzoni vijana wa Jangwani wangebeba taji la msimu huu mapema kabisa.

Ndiyo, Yanga imeongoza msimamo wa Ligi kwa muda mrefu hadi raundi ya kwanza ilipomalizika ikiiacha Simba kwa tofauti na pointi nane kabla ya Wekundu hao kuzipunguza kupuitia mechi za viporo iliyocheza mwezi ulioopita na kufanya pengo lisaliwa na pointi moja tu kwa sasa.


KAMA 2016-2017

Kwa wasiojua msimu wa 2016-2017 Simba ilionekana ina nafasi kubwa ya kubeba ubingwa kwani ilimaliza duru la kwanza ikiwa kinara wa msimamo ikikusanya pointi 35, mbili zaidi na ilizokuwa nazo Yanga iliyokuwa na 33, lakini mechi ya mwisho iliyopigwa Mei 20, Yanga ilibeba taji mbele ya Simba.

Msimu huo, Yanga ilibeba ubingwa kwa tofauti na mabao ya kufunga na kufungwa mbele ya Simba licha ya kila moja kumaliza na pointi 68 kwa kucheza mechi 30, kwani katika mechi mbili za mwisho kwa timu hizo, Yanga ilivuna pointi tatu tu, wakati Simba ilivuna sita, lakini mabao yanaiangusha.

Yanga ilishinda 2-1 dhidi ya Mbeya City na kupoteza 1-0 kwa Mbao FC wakati Simba yenyewe ilishinda zote kwa mabao 2-1 dhidi ya Stand United na Mwadui za Shinyanga.

Yanga ilikamilisha mechi 30 ikiwa imeshinda 21, sare tano na kupoteza nne, huku ikifunga mabao 57 na kufungwa 14, wakati Simba nayo ilikuwa imeshinda mechi 21 pia, sare tano na kupoteza nne, lakini ikifunga mabao 50 na kufungwa 17 na hapo hesabu za vidole zikapigwa na Yanga kuwa bingwa.

Hali ilikuwa tofauti katika mechi za duru la kwanza, kwani Simba iliongeza msimamo ikicheza michezo 15, ikishinda 11 na kutoka sare mbili na kupoteza mbili, ikifunga mabao 26 na kufungwa sita tu, ilihali Yanga ilikuwa ya pili ikishinda mechi 10 kati ya 15 ilizocheza, ikitoka sare tatu na kupoteza mbili, huku ikifunga mabao 31 na kuruhusu manane kugusa nyavu zao kabla ya kupindua meza lala salama.


MTIHANI WA SIMBA

Japo mazingira ya msimu huu ni tofauti na ule wa 2016-2017, safari hii Simba inahitaji kushinda mechi zote tatu ilizonazo mkononi mwa sasa katika Ligi Kuu ili kubeba ubingwa, kwani pengo la pointi moja baina yao na Yanga ndilo linalowapa mtihani hata kama kila moja itashinda mechi mbili za awali.

Hata hivyo, kucheza na timu zilizoshuka daraja mapema KenGold ambao bado haijaingia kambini kujiandaa na mechi hiyo ya Jumatano na ile ya Kagera Sugar zinawapa wepesi Wekundu hao kulinganisha na Yanga inayovaana na Prisons inayopambana kuepuka kucheza mechi za play-off.

Ikitokea Yanga ikashinda nao mechi hizo mbili za mwisho ikiwamo dhidi ya Dodoma Jiji, itakuwa ikiombea ama itoke sare yoyote au kushinda itangaze ubingwa kwa msimu wa nne mfululizo, kinyume cha hapo Simba, ikishinda itakuwa imepoteza taji dakika za jioni.

Ushindi wa Simba kwa mechi zote tatu ikiwamo Dabi ya Juni 25 itaifanya ivune jumla ya pointi 81 na kuipiku Yanga itakayomaliza na 79 kama itashinda mbili za awali na kuchemsha Dabi ya Kariakoo na hiyo ndio sapraizi ambayo mashabiki wa soka wanaisubiri kuona kama upepo wa ubingwa utabadilika.


MGOSI, CHAMBUA UBINGWA

Nyota wa zamani wa Yanga, Sekilojo Chambua alisema anaamini hakuna mechi rahisi kwa timu zote, hasa kwa Yanga kutokana na nafasi iliyonayo Tanzania Prisons kwa sasa.

“Kwa kawaida mechi zote zitakuwa ngumu, hasa kwa Yanga, kwa sababu hizo timu mbili ambazo zinacheza na Simba tayari zimeshuka daraja. Lakini hata kama zimeshuka, zinapaswa kupigania heshima. Tazama Ulaya, timu imeshuka lakini inamfunga bingwa tunatakiwa kufika huko pia,” alisema Chambua na kuongeza;

“Hivyo Yanga hawana mechi nyepesi, wanapaswa kufanya kazi kweli kweli, ila sidhani kama kuna mtu atadondosha pointi.”

Kwa upande wa mshambuliaji wa zamani wa Simba, Mussa Hassan Mgosi, alisema anaona presha ya mechi hizi ni sawa na fainali kwa pande zote mbili.

“Mechi hizi mbili zilizobaki kwa kila timu ni kama fainali. Hakuna nafasi ya kuruhusu makosa. Wote wanajua kilicho hatarini na naamini wataingia kwa mbinu, ari na nguvu kubwa zaidi kuliko kawaida. Ukikosea sasa, basi umejiondoa mwenyewe.”

Nyota mwingine wa zamani wa kimataifa aliyewahi kukipiga Yanga na Mtibwa Sugar, Credo Mwaipopo, alisema presha kubwa itakuwa kwa timu itakayocheza baadaye baada ya mwenzake kucheza mapema.

“Ukiwa timu ya pili kucheza, tayari unakuwa na mzigo wa kufuatilia matokeo ya mpinzani. Ukiona wameshinda, presha inapanda.”