Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Siku 47 za usajili wachezaji Zanzibar

USAJILI Pict

Muktasari:

  • Issa amesema usajili huo utahusisha washiriki wote wa mashindano yanayosimamiwa na bodi hiyo kuanzia ngazi za Mikoa, Wilaya hadi Taifa huku akizitaka klabu zikamilishe usajili ndani ya muda uliopangwa.

MTENDAJI Mkuu wa Bodi ya Ligi Zanzibar, Issa Kassim Ali, amesema dirisha la usajili wa wachezaji kuelekea msimu wa 2026-2027 linafunguliwa Julai 20, 2026 na kufungwa Septemba 5, 2026, hivyo litadumu kwa takribani siku 47.

Issa amesema usajili huo utahusisha washiriki wote wa mashindano yanayosimamiwa na bodi hiyo kuanzia ngazi za Mikoa, Wilaya hadi Taifa huku akizitaka klabu zikamilishe usajili ndani ya muda uliopangwa.

“Hatutakuwa na muda wa nyongeza baada ya kufungwa kwa dirisha la usajili, hivyo nasisitiza timu kutumia muda huo vizuri uliotengwa kuepuka changamoto wakati wa mashindano,” amesema. 

Ameeleza kuwa, kipindi hicho kitatoa fursa kwa timu kusajili wachezaji wapya, kufanya uhamisho pamoja nyaraka muhimu zinazohitajika kwa mujibu wa kanuni za mashi ndano. Vilevile, amesema Bodi ya Ligi imekamilisha maandalizi ya awali ya msimu mpya na kwasasa inaendelea kushirikiana na wadau kuhakikisha mashindano hayo yanafanyika kwa kuzing atia kanuni, sheria na ratiba zilizopangwa.

Usajili huo ni sehemu ya maandalizi ya msimu wa 2026-2027 Zanzibar.