Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sababu ya Masaka kubaki Brighton

MASAKA Pict

Muktasari:

  • Jeraha hilo lilitokea Novemba 8, 2024, wakati Masaka akicheza mechi yake ya kwanza ya Ligi Kuu ya Wanawake England (WSL) akiwa na Brighton & Hove Albion Women dhidi ya Arsenal Women. Aliingia kipindi cha pili, lakini dakika chache baadaye akapata jeraha lililomlazimu kutolewa kwa machela.

WIKIENDI iliyopita ilikuwa ya furaha kwa mashabiki wa soka la Tanzania baada ya mshambuliaji Aisha Masaka kurejea uwanjani kufuatia kukaa nje kwa muda mrefu akiuguza jeraha la bega alilopata katika mchezo dhidi ya Arsenal.

Jeraha hilo lilitokea Novemba 8, 2024, wakati Masaka akicheza mechi yake ya kwanza ya Ligi Kuu ya Wanawake England (WSL) akiwa na Brighton & Hove Albion Women dhidi ya Arsenal Women. Aliingia kipindi cha pili, lakini dakika chache baadaye akapata jeraha lililomlazimu kutolewa kwa machela.

Baada ya kipindi kirefu cha matibabu, inaelezwa kuwa viongozi wa Brighton walifikiria kumpeleka kwa mkopo mshambuliaji huyo ili apate nafasi ya kurejesha utimamu wake wa mwili na baadaye kurejea katika kikosi cha timu hiyo.

MASA 05

Hata hivyo, watu wanaomsimamia Masaka waliomba aendelee kubaki Brighton na kufanya mazoezi, licha ya kuwepo kwa ofa kutoka klabu mbalimbali zilizokuwa zikimhitaji.

Kwa mujibu wa kiongozi mmoja anayehusika na usimamizi wa mchezaji huyo, ambaye hakutaka jina lake litajwe, uamuzi huo ulilenga kumwezesha Masaka kuendelea kuwa karibu na mazingira ya soka na kujijenga upya, badala ya kuondoka klabuni akiwa bado katika hatua za kurejesha utimamu wake.

Chanzo hicho kilieleza kuwa kulikuwa pia na hofu ya athari za mashambulizi ya mashabiki kupitia mitandao ya kijamii, ambao walikuwa wakimkosoa mchezaji huyo. Watu wanaomsimamia waliona kuwa kuondoka Brighton katika kipindi hicho kungeweza kumweka mbali zaidi na ushindani wa soka. Hivyo, walishikilia msimamo wa kuendelea kubaki klabuni hapo, kufanya mazoezi na kusubiri mkataba wake ufike mwisho.

MASA 04

Changamoto ya mashabiki kutumia mitandao ya kijamii kuwashambulia wachezaji si jambo geni katika soka la Tanzania. Mwaka 2020, nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta, pia aliwahi kupitia kipindi ambacho mashabiki walikuwa wakiwashambulia wachezaji na timu kupitia mitandao hiyo.

Kwa Masaka, kurejea mazoezini Novemba 10, 2026, kunaashiria mwanzo wa ukurasa mpya baada ya kipindi kirefu cha kuuguza jeraha. Kwa sasa, jambo la msingi kwake ni kurejesha utimamu wa mwili, kupata nafasi ya kucheza na kujenga upya ushindani wake ili kurejea katika kiwango kilichomfanya Brighton imjumuisha kwenye kikosi chake.

MASA 03

Tangu alipojiunga na Brighton msimu uliopita akitokea BK Hacken ya Sweden, Masaka amecheza mechi mbili pekee, akikusanya dakika 14. Alitumia dakika nne dhidi ya Arsenal kabla ya kuumia, huku dakika 10 nyingine akizipata katika mchezo dhidi ya Birmingham.