Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Pogba: Kurudi Zanzibar haukuwa uamuzi sahihi

POGBA Pict

Muktasari:

  • Kabla ya mechi za jana, KVZ ilikuwa nafasi ya sita katika msimamo wa Ligi Kuu Zanzibar ikiwa na pointi 14, huku Zimamoto FC ikiwa kileleni na pointi 22.

KIUNGO mkabaji wa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Zanzibar, KVZ, Suleiman Juma Kidawa maarufu Pogba, amesema kwa sasa anaamini uamuzi wa kurejea kucheza Zanzibar baada ya kupata nafasi ya kuitumikia KMC katika Ligi Kuu Bara kabla ya kushuka daraja, haukuwa sahihi kwa mipango yake ya soka.

Kiungo huyo alicheza Ligi Kuu Bara kwa nusu msimu wa 2025-2026 akiwa na KMC iliyoshuka daraja, alitokea Mlandege na amerejea visiwani kuitumikia KVZ.

Amesema kwa sasa mipango na mikakati yake ni kurejea kucheza Ligi Kuu Bara na anataka kutumia nafasi inayofuata kurejea katika ushindani huo na anaamini bado kiwango chake kinamruhusu kucheza ligi hiyo.

“Sipo tayari kurudia uamuzi nilioufanya nilipokuwa KMC wa kurejea nyumbani. Kwa sasa naamini nilipaswa kuendelea kupambana na kutafuta nafasi nyingine ya kucheza Bara,” amesema.

Amesema ili kufanikisha mipango yake, lazima kwanza aisaidie KVZ kutetea taji lake la ligi na kutwaa Kombe la FA, akiamini hilo linawezekana kwa kushirikiana na wachezaji wenzake.

Pogba amesema dhamira yao ni kutetea ubingwa na kuhakikisha wanafanya vizuri katika michezo saba iliyobaki ili kumaliza mzunguko wa kwanza wakiwa ndani ya timu nne za juu.

Kabla ya mechi za jana, KVZ ilikuwa nafasi ya sita katika msimamo wa Ligi Kuu Zanzibar ikiwa na pointi 14, huku Zimamoto FC ikiwa kileleni na pointi 22.