Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Pep: Hakuna wa kumfananisha na Lionel Messi

Muktasari:

  • TOLEO lililopita, mwandishi Luca Caioli alielezea jinsi mastaa Messi na Ronaldo walivyouwasha moto msimu wa 2009/10 Messi akitamba na mataji ingawa Real ya Ronaldo haikuwa na msimu mzuri wakati Barcelona mambo yalipendeza. Endelea…

TOLEO lililopita, mwandishi Luca Caioli alielezea jinsi mastaa Messi na Ronaldo walivyouwasha moto msimu wa 2009/10 Messi akitamba na mataji ingawa Real ya Ronaldo haikuwa na msimu mzuri wakati Barcelona mambo yalipendeza. Endelea…

Hadi mwisho wa msimu Ronaldo akawa amefunga jumla ya mabao 33 licha ya kupata majeraha na kuwa nje ya uwanja kwa miezi miwili. Alifunga mabao 26 katika La Liga ikiwamo hat trick yake ya kwanza ya La liga katika mechi ya Real Madrid dhidi ya Mallorca iliyochezwa Mei, 5, 2010 pamoja na mabao saba katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Ronaldo alikuwa burudani kwa mashabiki wa Real Madrid, lakini pia alikuwa na wakati wa kuchukizwa na mambo, Real ilikuwa na msimu wa hovyo, katika ligi ya mabingwa iliishia hatua ya 16 bora, katika Kombe la Mfalme nako hali haikuwa vizuri na La Liga ilitawaliwa na Barcelona na Messi wao.

2010/11

Hali ikawa hivyo hivyo kwa Ronaldo katika msimu uliofuata (2010/11), akawa hashikiki, akawa mashine ya mabao, alifunga jumla ya mabao 53 na kutwaa tuzo ya mfungaji bora Ulaya.

Na kwa mabao yake 40 kwenye La Liga katika mechi 34 akaivunja rekodi ya Telmo Zarra wa Athletic Bilbao aliyefunga mabao 38 katika mechi 30 msimu wa 1950/51 pamoja na Hugo Sanchez wa Real aliyefunga mabao 38 katika mechi 35 msimu wa 1989/90.

Hata hivyo kwa mara nyingine Real wakaambulia taji moja tu baada ya kuifunga Barcelona katika Kombe la Mfalme, ni dhahiri taji hilo halikutosha kwa Ronaldo ambaye ana shauku ya kushinda makubwa.

“Real tulikuwa na shauku ya kushinda mataji yote na ningependa kufunga nusu ya mabao yote lakini hapo hapo nishinde mataji ya La Liga na Ligi ya Mabingwa Ulaya,’’ alisema Ronaldo alipozungumza na kituo kimoja cha redio.

Kwa kuangalia uwiano nyota yake binafsi ilikuwa ikipaa, “Najiona katika mazingira mazuri, na unaweza kusema kuwa huu ulikuwa msimu wangu bora.

Kimahesabu kwa kiwango chake cha uchezaji yeye na timu yake, Ronaldo alitoa alama nane au tisa kati ya 10 ingawa hakukuwa na ubishi kwamba Real na Ronaldo walikuwa na mwaka mgumu uliochangiwa na mahasimu wao, Barcelona ya Pep Guardiola na zaidi ya yote adui yao mkuu alikuwa Messi.

Messi alijipaisha juu zaidi, alifikia rekodi ya mabao ya Ronaldo, mabao 53. Katika Ligi ya Mabingwa Ulaya alikuwa kinara na mabao 1, idadi ambayo Ronaldo aliifunga Ruud van Nistelrooy msimu wa 2002/03 wakati huo akiwa na Man United.

Ndio kwanza ana miaka 23, kinara wa mabao katika ligi ya mabingwa kwa mara ya tatu hapo huzungumzii ushindi wa mataji 14 akiwa na jezi ya Barcelona. Namba hizo na mataji unaweza kuweka kando jambo la muhimu ni uwapo wa Messi, wakati wote ndiye aliyekuwa kinara wa kubadili mchezo.

Wakati wote alicheza katika ubora wake, ni nguzo muhimu katika timu yake hadi kutwaa taji lake la tatu la La Liga.

Na pengine la muhimu zaidi ni kwamba alifanikiwa kubeba taji lake la tatu la Ligi ya Mabingwa Ulaya, Mei 29, 2011 kwenye Uwanja wa Wembley baada ya kuifunga kwa mara nyingine Man United.

Akiwa katika makazi ya soka la England (Wembley), Messi alicheza kwa kiwango cha juu kilichovutia, Waingereza walitoka uwanjani wakifahamu kwamba wameshuhudia uzinduzi wa soka tamu na la kuvutia.

Aliwaachia mechi ya kuwahadithia wajukuu zao, mechi ambayo ilikuwa sababu ya kubeba misemo yote bora ya vyombo vya habari vya Uingereza.

Gazeti la The Times lilisema, ‘Utawala wa Mfalme Messi’ wakati The Guardian lilimfananisha na Nador Hidekuti, ambaye katika uwanja huo huo mwaka 1953 alipiga hat trick wakati Hungary ikiibugiza England mabao 6-3.

Katika mechi na Man United, Barcelona iliichapa Man United mabao 3-1, “ni mchezaji bora ambaye sijawahi kuona mfano wake na sitoona tena,’’ alisema Pep Guardiola mara baada ya mechi hiyo.

“Tuna uwezo wa kushindana katika kiwango cha juu, lakini bila ya yeye hatuwezi kucheza soka la hadhi ya juu, tumeonyesha kwamba tunamudu kufanya juhudi, tuna kipaji na tuna Messi, ni wa kipekee na hana wa kumfananisha naye.

Itaendelea Jumamosi ijayo…