Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Penalti ya jioni yaipa Mashujaa FC pointi tatu muhimu

Muktasari:

  • Katika mechi hiyo, ilishuhudiwa wenyeji, Mashujaa ikipata bao la kutangulia dakika ya 30, lililofungwa na mshambuliaji nyota wa kikosi hicho, Mishamo Michael dakika ya 30, akiunganisha mpira kwa kichwa pasi iliyopigwa na Haruna Chanongo.

BAO la dakika ya 90+5, la penalti ya mshambuliaji wa Mashujaa FC, Michael Joseph limetosha kuipa timu hiyo ushindi wa mabao 2-1, dhidi ya Polisi Tanzania, katika mechi ya Ligi Kuu Bara iliyopigwa kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma.

Katika mechi hiyo, ilishuhudiwa wenyeji, Mashujaa ikipata bao la kutangulia dakika ya 30, lililofungwa na mshambuliaji nyota wa kikosi hicho, Mishamo Michael dakika ya 30, akiunganisha mpira kwa kichwa pasi iliyopigwa na Haruna Chanongo.

Bao hilo liliipeleka Mashujaa FC hadi mapumziko ikiwa inaongoza, japo kipindi cha pili Polisi Tanzania ilirejea kwa kasi na kusawazisha dakika ya 52, lililofungwa kwa penalti na mshambuliaji nyota wa kikosi hicho cha maafande, Anuary Jabir.

Penalti hiyo ya Anuary, ilitokana na makosa yaliyofanywa na kiungo wa maafande wa Mashujaa FC, Tariq Simba aliyemchezea madhambi mchezaji wa Polisi Tanzania, Rajabu Athumani katika eneo la hatari, hivyo, kutumia nafasi nzuri ya kusawazisha. 

Anuary aliyejiunga na kikosi hicho msimu huu akitokea Dodoma Jiji, ameendeleza kiwango cha kuvutia na kikosi hicho baada ya kufikisha bao lake la sita msimu huu wa 2026-2027 la Ligi Kuu Bara, akiendelea kuongoza katika mbio za ufungaji bora.

Wakati mechi hiyo ikionekana kumalizika kwa sare ya 1-1, Mashujaa FC ilipata penalti ya dakika ya 90+5, iliyofungwa na mshambuliaji wa kikosi hicho, Michael Joseph na kukihakikishia kikosi hicho cha maafande kubaki na pointi tatu nyumbani.

Penalti hiyo iliamuliwa na Teknolojia ya Football Video Support (FVS), baada ya mchezaji wa Polisi Tanzania, Kenny Ally Mwambungu kuunawa mpira eneo la hatari na kuipa faida Mashujaa kupata bao lililofungwa na mshambuliaji, Michael Joseph.

Bao hilo ni la kwanza la Ligi Kuu Bara kwa nyota huyo tangu ajiunge na kikosi hicho, Julai 20, 2026, akitokea KVZ FC ya visiwani, Zanzibar, alipoibuka mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Zanzibar kwa msimu wa 2025-2026, baada ya kuonyesha kiwango kizuri.

Michael alikuwa mfungaji bora wa Ligi ya Zanzibar akiwa na KVZ FC, baada ya kufunga mabao 21 katika mechi 29, alizocheza akitumia dakika 2320 kwa msimu wa 2025-2026, huku akitoa pia asisti nane na kumfanya kuhusika kwenye jumla ya mabao 29.

Kiwango bora cha nyota huyo kiliiwezesha KVZ FC kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Zanzibar, baada ya kumaliza na pointi 67, nyuma ya JKU SC iliyomaliza ya pili na pointi 64 kwa msimu wa 2025-2026, jambo lililoivutia Mashujaa kuitaka saini yake.

Matokeo hayo yanaifanya Mashujaa FC kusogea hadi nafasi ya nne na kuishusha Singida Black Stars ikiwa na pointi zake 12, baada ya kushinda mechi nne na kutoka sare tatu kati ya saba ilizozicheza, huku ikifunga mabao manane na kuruhusu saba.

Kwa upande wa Polisi Tanzania iliyocheza mechi saba, imeshinda tatu, sare moja na kupoteza tatu, ikiwa nafasi ya saba na pointi 10 na kuishusha Dodoma Jiji kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa inayosogea hadi nafasi ya nane na pointi 10.