Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Pacome awekwa pembeni, Clement Mzize ndani

Muktasari:

  • Akizungumza na Mwanaspoti Msemaji wa Yanga Ally Kamwe alisema tayari wame-pewa maendeleo yake na daktari wa timu namna anavyoimarika kwa haraka.

BAADA ya mshambuliaji wa Yanga, Clement Mzize kukaa nje msimu mzima uliopita kutokana na kusumbuliwa na majeraha, taarifa za kufurahisha kwa mashabiki wa timu hiyo ni kwamba msimu ujao atakuwa sehemu ya kikosi.

Akizungumza na Mwanaspoti Msemaji wa Yanga Ally Kamwe alisema tayari wame-pewa maendeleo yake na daktari wa timu namna anavyoimarika kwa haraka.

“Niwape taarifa tu kwamba Mzize anaendelea vizuri, hivyo mtamshuhudia sana kwenye mechi za msimu ujao, tofauti na kile wengi wanadhani atahitaji muda wa kurejea taratibu,” alisema na kuongeza; “Kutokana na usajili wetu, watu mtandaoni wanasema tumesajili washambuliaji wengi watacheza wapi, niwajibu kwamba wa-tacheza kwenye timu yetu, Yanga itakuwa na wachezaji hatari, wanaocheza chuma, wanasubiri benchi chuma, atakayezembea tu, basi wajue imekula kwao wa-tasahaulika.” Mbali na Mzize alisema maendeleo ya nahodha Dickson Job pia yapo vizuri na atarejea kwenye ushindani, utakaofanya kikosi kiwe kipana.

Msimu wa 2024/25 Mzize alimaliza na mabao 14 na asisti 5, huku 2023/24 akifun-ga mabao 06 na asisti saba baada ya kusumbuliwa na majeraha.


KUHUSU PACOME

Alisema kutokana na majeraha aliyonayo kiungo mshambuliaji, Pacome Zouzoua, watamtoa katika mfumo wa usajili ili apate muda wa kutosha wa kujiuguza.

“Pacome ataendelea kupata stahiki kama wachezaji wengine, lengo atibiwe kika-milifu, ila akipona atarejeshwa kikosini,” alisema Kamwe.