Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Pacome ampiga benchi Andigra akianza Ivory Coast

PACOME Pict

Muktasari:

  • Pacome ambaye ni mara ya pili anaitwa kwenye kikosi cha Ivory Coast katika kikosi hicho kinachoanza ni mchezaji pekee anayecheza Afrika amepata nafasi ya kuanza, huku akimsugulisha benchi staa wa Sunderland, Simon Adingra anayecheza pia nafasi kama yake.

KIUNGO wa Yanga, Pacome Zouzoua amepangua kikosi cha kwanza cha timu yake ya taifa ya Ivory Coast, akianza huku akiwaacha nje mastaa wakubwa.

Pacome ambaye ni mara ya pili anaitwa kwenye kikosi cha Ivory Coast katika kikosi hicho kinachoanza ni mchezaji pekee anayecheza Afrika amepata nafasi ya kuanza, huku akimsugulisha benchi staa wa Sunderland, Simon Adingra anayecheza pia nafasi kama yake.

Kocha Emerse Fae kwenye kikosi hicho ukiondoa Pacome ameanza na wachezaji 10 ambao wote wanacheza mataifa mbalimbali Ulaya, kwenye mchezo huo wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia wa mechi za kundi F.

Kwenye kikosi hicho ukuta wa Ivory Coast unaundwa na kipa Alban Lafont(Panathanaikos,Ugiriki) mabeki wakiwa Sheriff Tiraspol (Iberia, Georgia), Willy Boly (Nottingham Forest, England), Emmanuel Agbadou (Wolverhampton Wanderers, England) na Christopher Operi (Istanbul Basaksehir, Uturuki)

Katika kikosi ambacho kitashuka uwanjani baadaye kucheza dhidi ya Shelisheli ugenini, Pacome ameanza sambamba na viungo wengine wawili Ibrahim Sangare anayeichezea Nottingham Forest ya England na winga Yan Diomande wa RB Leipzig ya Ujerumani.

Wamo pia winga Toure Bazoumana (TSG Hoffenheim, Ujerumani), huku washambuliaji wakiwa Oumar Diakite wa Cercle Brugge ya Ubelgiji na Evann Guessand wa Nice ya Ufaransa.