Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nyuma ya pazia kufukuzwa kwa makocha Zanzibar

MAKOCHA Pict

Muktasari:

  • Lakini nyuma ya matokeo hayo mabaya, imeelezwa kwamba, baadhi ya timu zinazoshiriki Ligi Kuu Zanzibar zimekuwa hazitoi mahitaji yanayowasilishwa na mabenchi ya ufundi.

KUTOKANA na ushindani uliopo kwenye Ligi Kuu Zanzibar (ZPL) huku zikichezwa raundi tisa, hadi sasa makocha watatu ndani ya ligi hiyo wamesitishiwa mikataba yao baada ya mfululizo wa matokeo mabaya.

Lakini nyuma ya matokeo hayo mabaya, imeelezwa kwamba, baadhi ya timu zinazoshiriki Ligi Kuu Zanzibar zimekuwa hazitoi mahitaji yanayowasilishwa na mabenchi ya ufundi.

Kocha wa kwanza alikuwa Juma Pweka aliyeionoa Wembe ambapo aliondolewa baada ya kupokea kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Uhamiaji.

Timu hiyo kwasasa inanolewa na Kocha Ally Manyani, hata hivyo, bado haijawa vizuri kwani tangu aichukue kafanikiwa kupata ushindi mmoja tu dhidi ya Fufuni.

UHA 01

Nayo Mwenge iliamua kuachana na Kocha Mkuu, Msellem Sultan Hemed baada ya vipigo vinne mfufululizo.

Katika mechi nne ilizocheza timu hiyo ikiwa na kocha huyo, matokeo yalikuwa kama yafuatavyo; Mwenge 0-2 Muembe Makumbi, Mwenge 1-2 Raskazone, Uhamiaji 2-0 Mwenge na Black Sailors 2-1 Mwenge.

Mwenge kwasasa inanolewa na Kocha Ali Kombo, ikiwa katika mstari wa kushuka daraja kwenye msimamo wa ligi hiyo nafasi ya 15 na imeshinda mechi moja pekee dhidi ya KVZ kwa bao 1-0.

Hivi karibuni uongozi wa timu ya Uhamiaji, ulifyeka benchi lote la ufundi lililokuwa likiongozwa na Kocha Mkuu, Sheha Khamis Rashid, Kocha Msaidizi, Hassan Makame Ameir na Kocha wa makipa Twahir Ahmada.

Licha ya kutoa taarifa kwa umma timu hiyo haikueleza sababu za kulifyeka benchi hilo lakini taarifa ilizonazo Mwanaspoti, uongozi huo haujaridhishwa na mwenendo wa matokeo kwa kupoteza mechi nne mfululizo.

UHA 02

Chanzo kutoka ndani ya timu hiyo kimeeleza kuwa, hakuna timu yenye malengo ambayo inaweza kuvumilia vipigo vinne mfululuzi ndio sababu kubwa ya kufukuza benchi hilo.

Mwanaspoti ilipata nafasi ya kuzungumza na mmoja wa makocha hao walioondolewa kwenye timu hizo, akidai viongozi wa klabu nyingi kisiwani hapa hawatoi mahitaji ambayo kocha anayapendekeza ndio sababu ya timu kufanya vibaya.

“Mara nyingi lawama zote zinakuja kwetu makocha lakini viongozi wa timu ndio chanzo cha matokeo mabovu kwani hawatoi wanachohitaji makocha,” amesema.

Kocha huyo, alidai kuwa kuna wakati kocha anahitaji mchezaji fulani lakini uongozi ukatafuta mbadala na matokeo yake yanakuwa hayo.

Amesema baadhi ya timu hazitoi posho kwa wachezaji jambo linawafanya baadhi yao kugoma au kujivunja kwa makusudi ili wasicheze.