Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba kutua Kenya kwa mechi ya kumbukumbu ya Raila Odinga

SIMBA Pict

Muktasari:

  • Timu hiyo itacheza mechi ya Ligi Kuu dhidi ya Namungo FC leo Jumatatu, ilikuwa ni ya mwisho kwa kikosi hicho kwa ajili ya kupisha Kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), jambo ambalo mabosi wa Simba wanataka kujipanga vizuri.

UONGOZI wa Simba unafanya mchakato wa kuweka kambi Kenya kwa ajili ya maandalizi ya mechi zijazo za Ligi Kuu Bara na Ligi ya Mabingwa Afrika, ikihitaji kutumia vizuri mapumziko kupisha Kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).

Timu hiyo itacheza mechi ya Ligi Kuu dhidi ya Namungo FC leo Jumatatu, ilikuwa ni ya mwisho kwa kikosi hicho kwa ajili ya kupisha Kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), jambo ambalo mabosi wa Simba wanataka kujipanga vizuri.

Taarifa kutoka Kenya, zinadai Simba imepata mualiko wa kushiriki Raila Odinga Cup, kwa lengo la kumbukizi ya aliyekuwa Waziri Mkuu, Raila Amolo Odinga aliyefariki dunia Jumatano ya Oktoba 15, 2025, wakati akipatiwa matibabu huko, India.

Katika mualiko huo wa kutimiza mwaka mmoja tangu kifo cha Odinga, itachezwa mechi ya kirafiki kati ya kikosi hicho cha Simba ya Tanzania dhidi ya Gor Mahia FC ya Kenya, inayotarajiwa kuchezwa Novemba 15, 2026, ili kumkumbuka kiongozi huyo.

Hii itakuwa ni mara ya pili kwa Simba kuweka kambi nje ya nchi katikati ya msimu wa 2026-2027, baada ya kufanya hivyo, Septemba 24, 2026, ilipokwenda katika Mji wa Polokwane uliopo Jimbo la Limpopo huko, Afrika Kusini na kukaa kwa siku 10.

Kambi hiyo ya siku 10, ya Afrika Kusini, ilikuwa na manufaa kwa kikosi hicho, kwani iliporejea Oktoba 4, 2026, mechi ya kwanza baada ya mapumziko ya FIFA, ilicheza na watani zao wa jadi Yanga na kuifunga mabao 2-1, Oktoba 10, 2026. 

Mechi ya ‘Kariakoo Derby’, iliamsha hamasa zaidi kwa timu hiyo kwani hadi sasa haijapoteza Ligi Kuu Bara, ikiwa ni mwenendo mzuri ulioifanya kuingia hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika mara saba kwenye historia yake.

Kambi hiyo ni kwa lengo la kutengeneza utulivu wa wachezaji ambao hawajapata nafasi ya kuitwa katika timu zao za taifa, ili kujiandaa na mechi zijazo za Ligi Kuu Bara na ligi ya Mabingwa Afrika.