Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nabi aondoka Raja Casablanca

NABI Pict

Muktasari:

  • Nabi anaondoka Raja Casablanca akiwa ameinoa timu hiyo kwa siku 81 tu tangu alipojiunga nayo, Juni 12, 2026.

Kocha wa zamani wa Yanga, Nasreddine Nabi ametangaza kuachana na Raja Casablanca ya Morocco, jana Jumatatu, Agosti 31, 2026.

Nabi anaondoka Raja Casablanca akiwa ameinoa timu hiyo kwa siku 81 tu tangu alipojiunga nayo, Juni 12, 2026.

Inatajwa kwamba Raja Casablanca imeamua kuachana na Nabi kufuatia kocha huyo kutoridhishwa na Mkurugenzi wa Michezo, Rogerio Matias.

“Nilianza msimu mpya nikiwa na maono yaliyo wazi, malengo makubwa na hamu ya kujenga mradi unaoendana na kile ambacho Raja inawakilisha.

“Awali, maono haya yalishirikishwa na uongozi pamoja na wajumbe mbalimbali wa klabu na ilikuwa kwa msingi huo kwamba nilikubali mradi huu.
Hata hivyo, kadiri mradi huo na machaguo ya kimichezo yalivyokuwa yakibadilika, baadhi ya mielekeo nayo ilibadilika, na hatimaye maono yetu kuhusu namna ya kujenga mwendelezo wa mradi huo yakatofautiana.

“Ninaheshimu kikamilifu uamuzi huu na sitaki tofauti za kimtazamo kuhusu masuala ya kimichezo zigeuke kuwa mabishano au mjadala wa utata. Raja iko juu yetu sote. Nilipowasili, nilisema kwamba timu haiwezi kumtegemea mtu mmoja. Bado ninaamini hivyo. Kocha, mchezaji au mtu mwingine yeyote hayuko, wala hatakuwa, juu ya taasisi ya klabu,” amesema Nabi.

Tayari Raja Casablanca imeshapata kocha wa kuziba pengo la Nabi ambapo wamemchukua Mhispania Paco Jemez.