Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mzize: Kundi gumu lakini subirini muone

MZIZE Pict


LICHA ya kutokuwa sehemu ya kikosi kilichosafiri kwenda Algeria kwa mechi ya pili ya makundi dhidi ya JS Kabylie, mshambuliaji Clement Mzize amewasifu wenzake kwa kuanza vizuri nyumbani na kuwatumia salamu na  kuwataka wafanye vyema ugenini ili waende robo fainali.


Mzize amesema watakapofanya vyema katika mechi hiyo ya leo watakuwa na kila sababu ya kuisaka robo fainali baada ya msimu uliopita kukwama kidogo mbele ya Al Hilal na MC Alger na anaamini wenzake wana njaa ya mafanikio licha ya kukosekana kwake.


Akizungumza na Mwanaspoti, Mzize amesema licha ya ugumu wa kundi B lenye AS Far Rabat ya Morocco na Al Ahly, huku  mengi yakizungumzwa juu ya mwanzo mbovu wa timu hiyo, lakini anaiona Yanga ikifanya vizuri na amekaa na wachezaji wenzake baada ya kuibutua Rabat, mechi iliyopigwa Zanzibar na kuwaeleza walipopatia na walipokosea ili wasirudie dhidi ya JS Kabylie.

NOND 02

“Nashukuru wameniahidi kutoniangusha na kuwaangusha Wanayanga kwa mechi hiyo ya ugenini, naamini Yanga itafika mbali zaidi ya msimu uliopita licha ya ugumu wa Kundi B,” amesema Mzize aliyepo nje ya uwanja akiuguza jeraha la goti alilolipata katika mechi ya awali dhidi ya Wiliete Benguela ya Angola na kushinda ugenini kwa mabao 3-0.

Amesema anaimani kubwa na timu hiyo kutokana na wachezaji waliopo kuwa na uchu wa mafanikio na aliumizwa na kauli hawawezi kufika popote kutokana na ugumu wa kundi.

NOND 03

“Yanga ina wachezaji wazuri, wanacheza kwa kasi na morali kubwa, nafikiri kilichobaki ni kuwaombea na kuwaamini kwa kazi wanayoifanya, wanatamani kuona wanakuwa bora zaidi ya walipo sasa, mechi ijayo itakuwa bora zaidi na watafanya vizuri.”

“Ushindi walioupata nyumbani umeongeza morali. Nipo Dar es Salaam lakini akili yangu ipo Algeria nawaza ni namna gani wapambanaji wenzangu watafanya kitu bora na cha kuwashangaza ambao hawaamini,” amesema Mzize aliyemaliza msimu uliopita akiwa kinara wa mabao wa klabu akifunga 14 ya Ligi Kuu Bara, mawili ya Ligi ya Mabingwa Afrika na mengine mawili ya FA.

NOND 04

Mzize aliyetwaa tuzo ya bao bora Afrika hivi karibuni, amesema kwa sasa anaendelea na mazoezi akifuata programu aliyopewa na daktari na anaamini atarudi mapema zaidi ya siku alizopewa kutokana na kuzingatia maagizo na anatamani kurudi kuipambania timu yake.