Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mzimu wa kadi nyekundu waitesa Simba, ikiilaza Singida BS

Muktasari:

  • Katika mechi ya leo iliyopigwa kwenye Uwanja wa Airtel Singida, Mligo alionyeshwa kadi hiyo nyekundu dakika ya 84, baada ya kumkanyaga kwa nyuma, Yusuph Khamis na kikosi hicho kufikisha wachezaji wa tatu hadi sasa msimu huu kwenye Ligi Kuu.

MZIMU wa kadi nyekundi umeendelea kuitesa Simba katika Ligi Kuu Bara, baada ya beki wa kushoto, Anthony Mligo kuonyeshwa leo na kufikisha tatu katika kikosi hicho kilichoibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Singida Black Stars.

Katika mechi hiyo iliyopigwa kwenye Uwanja wa Airtel Singida, Mligo alionyeshwa kadi hiyo nyekundu dakika ya 84 baada ya kumkanyaga  Yusuph Khamis na kikosi hicho kufikisha wachezaji watatu msimu huu kwenye ligi hiyo.

Kadi hiyo ilitokana na usaidizi wa Teknolojia ya Football Video Support (FVS). Mligo alimkanyaga  mshambuliaji wa Singida Black Stars, Yusuph Khamis wakati akiwa katika harakati za kushambulia.

David Kameta 'Duchu' alikuwa ni mchezaji wa kwanza wa Simba kuonyeshwa kadi nyekundu msimu huu katika ushindi wa kikosi hicho wa mabao 2-0, dhidi ya Kagera Sugar Agosti 16, 2026 baada ya nyota huyo kumchezea madhambi nahodha, David Luhende.

Mzimu wa kadi nyekundu ukaendelea tena kwa timu hiyo baada ya kiungo raia wa Nigeria, Ibraheem Jabaar kuonyeshwa katika ushindi wa kikosi hicho wa mabao 2-1, dhidi ya Pamba Jiji, Agosti 19, 2026, kwa kumchezea madhambi, Abdulkarim Yunus.

Katika mechi ya leo, Simba ilikuwa ya kwanza kupata bao lililofungwa na kiungo mshambuliaji, Clatous Chama dakika ya 12, baada ya nyota huyo kutumia vyema pasi ya Libasse Gueye, ambaye amefikisha asisti nne za Ligi Kuu Bara akiwa anaongoza.

Wenyeji Singida ilisawazisha bao hilo kunako dakika ya 23, kupitia kwa kiungo, Shekhan Khamis aliyetumia makosa ya kipa wa Simba, Hussein Abel aliyetokea kuudaka mpira uliopigwa na Mkongomani Jeancy Mboma Kinda na kumkuta mfungaji huyo.

Licha ya Teknolojia ya Football Video Support (FVS), kuonekana kuiumiza Simba kutokana na kadi nyekundu ya Mligo, ila iliinufaisha dakika ya 62, baada ya kikosi hicho kupata bao la penalti lililofungwa na beki wa kati, Rushine De Reuck.

Penalti hiyo iliamuliwa kwa msaada wa Teknolojia ya Football Video Support (FVS), baada ya beki wa Simba, Ismael Olivier Toure kufanyiwa madhambi eneo la hatari na kiungo wa Singida, Ahmed Pipino kisha mwamuzi, Ally Mnyupe kuamuru pigo hilo.

Ushindi huo unaifanya Simba kufikisha pointi zake tisa katika mechi tatu ilizocheza hadi sasa na kujikita kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Bara na kuishusha Yanga yenye pointi sita, ingawa mabingwa hao watetezi wamecheza mechi zao mbili.

Simba imeendeleza ubabe kwa Singida kwani mara ya mwisho zilipokutana kwenye Uwanja wa Airtel, Machi 11, 2026, ilishinda pia kwa mabao 2-1, yaliyofungwa na Alain Anicet Oura na Elie Mpanzu, huku lile la Singida likifungwa na Mossi Nduwumwe.