Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mwenge yapata ushindi wa kwanza ZPL

Muktasari:

  • Mechi hiyo ilichezwa Septemba 29, 2026 kwenye uwanja wa Mao A kisiwani Unguja, KVZ ilianza kuonyesha makali yake, lakini kadiri muda ulivyokuwa unakwenda, Mwenge ikawa inaimarika.

MWENGE SC imejiondoa kwenye kundi la timu ambazo hazijapata ushindi katika Ligi Kuu Zanzibar (ZPL) msimu huu baada ya juzi kuwachapa mabingwa watetezi wa ligi hiyo, KVZ bao 1-0.

Mechi hiyo ilichezwa Septemba 29, 2026 kwenye uwanja wa Mao A kisiwani Unguja, KVZ ilianza kuonyesha makali yake, lakini kadiri muda ulivyokuwa unakwenda, Mwenge ikawa inaimarika.

Ibrahimu Mgau ndiye aliyeipa Mwenge ushindi huo alipofunga bao dakika ya 23 lililoifanya lidumu hadi mwisho na kuipa timu hiyo pointi tatu ugenini zilizoifanya kutoka mkiani mwa msimamo wa ligi hadi kushika nafasi ya 14 kabla ya mechi za jana.

Kati ya mechi sita ambazo Mwenge imecheza, imeshinda moja, sare moja na kupoteza nne huku ikikusanya pointi nne.

Mwenge haikuanza vizuri msimu huu, kutokana na mfululizo wa matokeo mabaya, uongozi wa timu hiyo uliamua kuachana na aliyekuwa Kocha Mkuu, Msellem Sultan Hemed.

Matokeo ya mechi hizo sita za Mwenge yapo hivi; Mwenge 0-2 Muembe Makumbi, Mwenge 1-2 Raskazone, Uhamiaji 2-0 Mwenge, Black Sailors 2-1 Mwenge, Polisi 0-0 Mwenge na KVZ 0-1 Mwenge.

Kwenye mchezo mwingine uliochezwa juzi Jumanne, Fufuni imeendelea kuteseka kwa kufungwa mabao 2-1 na Polisi ambapo Recocatus Mayuya aliitangulizia Fufuni akifunga dakika ya 53, kisha Keya Ramadhan akaisawazishia Polisi dakika 58, kabla ya Mwinjuma Msoma kuongezea la pili dakika ya 72.  Ushindi wa Mwenge umeifanya kujiondoa kwenye orodha ya timu ambazo hazijapata ushindi katika ligi hiyo ambapo kabla ya mechi za jana, zilibaki tatu ambazo ni Mafunzo, Fufuni na KMKM.


MAFUNZO BADO INAJITAFUTA

LICHA timu ya Mafunzo kufanya mabadiliko makubwa ya kikosi msimu wa 2026-2027, lakini bado haijaonesha makali yake hadi kufikia sasa zaidi ya kukusanya pointi kupitia sare nne ilizopata, huku ikishindwa kuondoka na ushindi katika mechi tano ilizocheza.

Timu hiyo msimu uliopita 2025-2026 ilionekana kuwa na shida kubwa eneo la ushambuliaji ambapo ilimaliza na mabao 34 katika mechi 30, hali iliyolazimu uongozi wa klabu hiyo kufanya usajili kuboresha eneo hilo kwa msimu huu.

Hata hivyo, bado washambuliaji hawajatoa kile ambacho kinatarajiwa kufuatia kufunga mabao matatu katika mechi tano, huku mbili kati ya hizo dhidi ya Polisi na Muembe Makumbi zikiisha bila kufungana. Ilipocheza dhidi ya KMKM matokeo yalikuwa 1-1 kama ilivyokuwa dhidi ya Kipanga, huku ikipigwa 2-1 na Zimamoto.

Mabao matatu ya timu hiyo yamefungwa na washambuliaji wawili, Godfrey Kumbuka Mwailonda na Ramadhan Juma Matangalu, lingine likitokea kwa kiungo Kassim Suleiman Mikidadi. Washambuliaji wengine wa kikosi hicho ni Abdul Hakim Naim, James Mlange, Ikram Katembo na Abdallah Alagwa Ndame ambao hawajafunga.

Hivi karibuni, timu hiyo ilitambulisha Kocha Mkuu mpya, Innocent Alfred Mwamgonde aliyechukua nafasi ya Salum Haji kurejesha heshima na ushindi lakini bado mzigo mzito unaonekana kuwa upande wake.

Presha inaendelea kuongezeka ndani ya kikosi cha Mafunzo baada ya timu hiyo kujikuta ikikwama kupata ushindi badala yake kuandikisha matokeo ya sare katika michezo minne mfululizo ya Ligi Kuu ya Zanzibar.