Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mwamuzi ni yuleyule wa faulo

Muktasari:

BAADA ya Klabu ya Yanga kutoa malalamiko ya kutokuwa na imani na mwamuzi wa pambano la fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) kati timu hiyo na ya Simba, kamati ya waamuzi imeibuka na kutolea ufafanuzi juu ya kile kinachoendelea na kudai kuwa suala lao halina mashiko.

BAADA ya Klabu ya Yanga kutoa malalamiko ya kutokuwa na imani na mwamuzi wa pambano la fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) kati timu hiyo na ya Simba, kamati ya waamuzi imeibuka na kutolea ufafanuzi juu ya kile kinachoendelea na kudai kuwa suala lao halina mashiko.

Taarifa iliyotolewa na Yanga kupitia Idara ya Habari na Mawasiliano ilisema uongozi wa klabu hiyo umeshtushwa na chaguo la mwamuzi Ahmed Arajiga aliyepangwa kwa ajili ya kuchezesha mchezo wa fainali ya Kombe la ASFC utakaofanyika mjini Kigoma kesho Jumapili.

Yanga wanalalamika kwamba mwamuzi huyo amekuwa akichezesha mechi nyingi za Simba hasa kwenye kombe hilo ambako kachezesha mbili mfululizo.

Arajiga maarufu kama mwamuzi wa faulo kama alivyopewa na mashabiki mitandaoni, alivuma zaidi baada ya kuruhusu faulo ya harakaharaka kwenye mechi ya nusu fainali iliyoikutani Simba na Azam na kuzaa bao pekee lililoivusha Simba kutinga hatua ya fainali.

Bao hilo la Luis Jose lililalamikiwa na Azam ingawa mwamuzi alisema kikanuni ni sawa na kuungwa mkono na mamlaka za soka.

Chanzo cha bao hilo ilikuwa ni faulo aliyofanyiwa Bernard Morrison aliyekuwa akienda kumuona kipa wa Azam, Mathias Kigonya, ambapo mwamuzi aliamuru ipigwe.

Hata hivyo, wakati wachezaji wa Azam wakimlalamikia mwamuzi juu ya faulo hiyo, Morrison alipiga mpira harakaharaka na Luis kuukwamisha wavuni, suala ambalo liliibua malalamiko kutoka kwa wachezaji wa wa Azam na pia kuibua mijadala katika vyombo vya habari na mitandaoni.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi Tanzania (FRAT), Soud Abdi akizungumzia malalamiko hayo ya Yanga, alisema kuwa hoja zilizowasilishwa na wana Jangwani hazina mashiko kwani wao wamezingatia zaidi ubora wa mwamuzi na si kwa ajili ya kuipendelea timu fulani kama uongozi wa timu hiyo unavyodai kupitia malalamiko yake.

“Sisi kama kamati ya waamuzi tumezingatia ubora wa mwamuzi Arajiga kutokana na kiwango bora alichokionyesha kwenye michezo iliyopita,” ilisema taarifa ya kamati hiyo na kuongeza kuwa:

“Hivyo, kutokana na mchezo wenyewe jinsi ulivyokuwa mkubwa na unaobeba maslahi mapana ya watu tumeona ni vyema kumpa Arajiga kwa kuwa tunatambua wazi kuwa ataweza kulimudu pambano hilo vizuri.”

Sudi alisema katika taarifa yake kuwa licha ya presha iliyopo kwa sasa kuhusiana na mwamuzi huyo, lakini wao kama kamati hawana sababu ya kufanya mabadiliko kwa kuwa wamemteua kwa kutumia vigezo vingi tofauti na waamuzi wengine.

“Kuchezesha mechi nyingi za timu moja kwa mwamuzi sio kigezo cha kufanya mwamuzi kuwa na mapenzi na timu fulani, bali tumechagua kutokana mchezo wenyewe ulivyo na tumeona anamudu, hivyo hatuna sababu ya kuteua mwamuzi mwingine,” ilisisitiza taarifa hiyo.

Katika mchezo huo mwamuzi Ahmed Arajiga atasaidiwa na washika vibendera Fedinand Chacha wa Mwanza na Mohamed Mkono kutoka Tanga, huku mwamuzi wa akiba akiwa ni Elly Sasii kutoka jijini Dar es Salaam.

Simba na Yanga tayari ziko mjini Kigoma baada ya kutua juzu kwa ajili ya pambano hilo la kesho.