Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mwamba kastaafu, Aziz KI, Okello wanabaki na urithi

Muktasari:

  • Jana Jumanne, Oktoba 6, 2026, Messi alicheza mechi yake ya mwisho akiwa na Argentina, ikiifunga Benin mabao 3-0 katika mchezo maalumu wa kumuaga kwenye Uwanja wa Monumental jijini Buenos Aires. Nahodha huyo alifunga bao moja na kutoa pasi mbili za mabao, akimaliza safari yake ya kimataifa akiwa na mabao 126 na mechi 208.

WAKATI nyota wa soka duniani, Lionel Messi, akifunga ukurasa wa miaka 21 ya kuitumikia timu ya taifa ya Argentina, kuna wachezaji ambao safari zao za soka zimejengwa kwa kuvutiwa na ufundi wake. Miongoni mwao ni viungo wawili waliowahi kuvaa jezi ya Yanga, Stephane Aziz Ki na Allan Okello.

Jana Jumanne, Oktoba 6, 2026, Messi alicheza mechi yake ya mwisho akiwa na Argentina, ikiifunga Benin mabao 3-0 katika mchezo maalumu wa kumuaga kwenye Uwanja wa Monumental jijini Buenos Aires. Nahodha huyo alifunga bao moja na kutoa pasi mbili za mabao, akimaliza safari yake ya kimataifa akiwa na mabao 126 na mechi 208.

Messi anaondoka kwenye timu ya taifa akiwa ameacha alama kubwa, ikiwamo kuiongoza Argentina kutwaa Kombe la Dunia mwaka 2022 na mataji mawili ya Copa America mwaka 2021 na 2024. Safari hiyo imekuwa funzo kwa kizazi cha wachezaji waliokulia wakimtazama akicheza.


AZIZ KI

Kiungo wa Burkina Faso, Stephane Aziz Ki, aliwahi kueleza katika mahojiano na Mwanaspoti kuwa wachezaji waliomvutia na kumwelekeza katika mchezo wa soka ni Juan Roman Riquelme, Lionel Messi na Luka Modric.

Aziz Ki alieleza kuwa nafasi anayopendelea kucheza ni kiungo mshambuliaji, namba 10, akipenda zaidi kutengeneza nafasi za mabao kwa wenzake kuliko kujikita katika kufunga pekee.


OKELLO

Kwa upande wake, Allan Okello, kiungo mshambuliaji raia wa Uganda, naye aliwahi kueleza namna Messi anavyomvutia, hasa katika uwezo wake wa kutumia mguu wa kushoto.

Katika mahojiano Mwanaspoti, Okello alisema amekuwa akimtazama Messi kwa muda mrefu na kuvutiwa na kipaji chake, akitaja pia Andres Iniesta na Kevin De Bruyne miongoni mwa wachezaji anaowafuatilia.


HISTORIA YA MESSI

Messi alizaliwa Juni 24, 1987, mjini Rosario, Argentina. Alianza kung’ara akiwa Barcelona, ambako alijijengea historia kupitia mabao, pasi za mwisho na mataji mbalimbali kabla ya kuhamia Paris Saint-Germain na baadaye Inter Miami ya Marekani.

Katika maisha yake ya soka, ametwaa tuzo saba za Ballon d’Or kwa mujibu wa rekodi za Barcelona, akishinda pia mataji makubwa ya klabu na timu ya taifa.

Safari yake na Argentina haikuwa rahisi mwanzoni, lakini mafanikio ya Copa America 2021 na Kombe la Dunia 2022 yaliimarisha nafasi yake katika historia ya soka la nchi hiyo.