Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mtunisha misuli aahidi jambo

MISULI Pict

Muktasari:

  • Mwandemele aliyasema hayo baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, akitokea Zimbabwe alikoshiriki mashindano ya kimataifa ya mchezo huo, huku akieleza kuwa mafanikio hayo ni ishara ya uwezo wa Watanzania kufanya vizuri wanapopata nafasi na maandalizi yanayostahili.

BINGWA wa mashindano ya kimataifa ya ujenzi wa mwili, Abraham Mwandemele, maarufu kama Cobra the Beast, amesema hakuna kitu kinachoweza kumzuia kutimiza malengo yake, akiahidi kuiletea Tanzania Pro Card katika mashindano yajayo yatakayofanyika Afrika Kusini, Desemba mwaka huu.

Mwandemele aliyasema hayo baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, akitokea Zimbabwe alikoshiriki mashindano ya kimataifa ya mchezo huo, huku akieleza kuwa mafanikio hayo ni ishara ya uwezo wa Watanzania kufanya vizuri wanapopata nafasi na maandalizi yanayostahili.

Bingwa huyo amesema yeye ni mshindi na kila anapokwenda kushiriki mashindano, wapinzani wake wanapaswa kujiandaa kukabiliana naye.

“Mimi ni mshindi, sehemu yoyote nitakayokanyaga mguu wao waanze kujua watanikanyaga vipi, si mimi ninayekanyaga vipi. Ni bingwa, hakuna kitu cha kunizuia na sioni kitu chochote kitakachonizuia,” amesema Mwandemele.

Amesema ushindi wake una maana kubwa si kwake pekee, bali pia kwa vijana wengine nchini wanaotamani kufikia mafanikio kupitia mchezo wa ujenzi wa mwili, akisisitiza kuwa wanahitaji kuamini katika uwezo wao na kuendelea kupambana licha ya changamoto zinazoweza kujitokeza katika safari ya kutimiza ndoto zao.

Akizungumzia hatua inayofuata, Mwandemele amesema sasa anajiandaa na mashindano ya Pro Qualifier yatakayofanyika Afrika Kusini mwezi Desemba, ambako analenga kupata Pro Card.

“Ninachowaahidi ni kwamba mwezi wa 12 kuna mashindano ya Pro Qualifier yanayofanyika Afrika Kusini, nawaletea Pro Card,”amesema.

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Ujenzi wa Mwili Tanzania (TBDF), Francis Mapugilo, alimpongeza Mwandemele kwa mafanikio hayo na kuishukuru Serikali kwa kuwezesha wanamichezo wenye sifa kushiriki mashindano ya kimataifa.

“Ushindi wa Cobra the Beast ni ushindi wa taifa. Tunashukuru kwa sababu kila anapokwenda anafanya mambo yanayoonyesha kuwa ujenzi wa mwili ni mchezo unaohitaji kuendelezwa, hasa kwa vijana,”  amesema Mapugilo.

Mwandemele ameongeza kuwa mafanikio yake yanapaswa kuwa chachu kwa vijana wengine, akisema Tanzania ina uwezo wa kutoa wanamichezo wengi watakaofanya vizuri kimataifa endapo watapata sapoti inayohitajika.”