Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mtego wa Rushine unaomjenga Masinde

MASINDE Pict


BEKI wa kati wa Simba, Vedastus Masinde amesema kucheza pamoja na Rushine De Reuck, raia wa Afrika Kusini, kunamfanya ajifunze vitu vingi kutoka kwake vitakavyomsaidia kukua katika misingi ya ushindani, nidhamu na ukomavu.


Masinde huu ni msimu wake wa kwanza kucheza Ligi Kuu baada ya Simba kumsajili kutoka TMA FC ya Arusha inayoshiriki Ligi ya NBC Championship pia alikuwa anacheza timu ya taifa ya U20, Ngorongoro Heroes.


Amesema Rushine, aliyeifungia Simba mabao matatu, ana uzoefu na timu alizopitia kama Mamelodi Sundowns, jambo linalodhihirisha nidhamu yake, vinginevyo asingekuwa anacheza kwa kiwango alichonacho kwa sasa.

MASI 01

“Ingawa najifunza kwa wachezaji tofauti Simba, lakini Rushine ninayecheza naye nafasi moja, tukiwa tunafanya mazoezi anawapa changamoto nzuri washambuliaji kama vile tunacheza na timu pinzani, licha ya kuwa na jina kubwa, anajituma kwa bidii kama vile anatafuta nafasi ya kikosi cha kwanza au kuonekana, kitu hicho kinanipa nguvu ya kujituma bila kuchoka,” amesema Masinde na kuongeza:

“Kitu kingine alichonacho Rushine ni nidhamu ya muda, iwe wakati wa kwenda mazoezini au muda wa kupata chakula na kupumzika, siyo mchezaji anayejivuta na amekuwa akinisisitiza nizingatie muda kama nataka nifike mbali.”

MASI 02

Jambo lingine alilosema amekuwa akiambiwa mara kwa mara na Rushine ni kwamba wakati anazipambania ndoto zake, aendelee kusimamia misingi inayotakiwa katika mpira wa miguu ambayo itamsaidia kumpa mwongozo wa kile anachokitamani katika maisha yake.

Kwa upande wa kocha wa timu hiyo, Steve Barker amesema Masinde ana kitu kikubwa na kadri anavyoendelea kukua ndivyo atakavyofanya mambo makubwa katika mpira wa miguu: “Ni beki mzuri aliye na vitu vingi mguuni, kadri anavyopewa nafasi ndivyo anavyozidi kuimarika kiuchezaji.”

MASI 03

Kwa baadhi ya mechi alizocheza na kuanza ni dhidi ya Tanzania Prisons, Dodoma Jiji na Mashujaa, mechi alizokuwa benchi wakati Rushine De Reuck akianza ni dhidi ya Coastal Union na TRA United, jambo ambalo kocha Barker alisisitiza kwamba Masinde alifanya kazi nzuri.

Masinde amesema: “Kocha amekuwa akiniambia mimi ni mchezaji mzuri, niendelee kujifunza, kujituma na kuongeza bidii ili nije kufanya mambo makubwa.”

Mbali na hilo, Masinde ni miongoni mwa wachezaji waliopo katika timu ya taifa ya Serengeti Boys iliyotolewa kwa penalti 4-2 dhidi ya Senegal katika mechi ya fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 (AFCON U-17), mechi iliyopigwa mjini Rabat, Morocco.