Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mtanzania ang’ara Barcelona

BARKA Pict

Muktasari:

  • Barka, anayekipiga katika akademi ya FC Barcelona, ameng’ara katika mashindano hayo yanayoendelea kwa kushirikisha baadhi ya akademi kubwa za Ulaya.

MTANZANIA Barka Seif Mpanda anayekipiga katika akademi ya FC Barcelona iitwayo La Masia, ameonekana kufanya vizuri kwenye mashindano ya Virgil Legacy Trophy baada ya kufunga mabao matatu na kutoa asisti moja katika michezo miwili ya mashindano hayo.

Barka, anayekipiga katika akademi ya FC Barcelona, ameng’ara katika mashindano hayo yanayoendelea kwa kushirikisha baadhi ya akademi kubwa za Ulaya.

Katika michezo ya juzi, Barka alifunga bao moja wakati Barcelona ilipokutana na vijana wa Chelsea, kabla ya kuongeza mabao mawili na kutoa asisti moja katika mchezo mwingine dhidi ya Willem II ya Uholanzi.

Kiwango hicho kimemsaidia kumaliza hatua ya makundi akiwa miongoni mwa vinara wa Kundi A, ambalo pia lina akademi za Chelsea, Willem II na Galatasaray.

BAR 01

Mashindano hayo yameanzishwa na kusimamiwa na beki wa Liverpool, Virgil van Dijk, kwa lengo la kuwakutanisha vijana kutoka akademi mbalimbali na kuwapa nafasi ya kujifunza na kushindana katika mazingira ya kiwango cha juu.

Lakini kabla ya kuanza kuonekana kwenye mashindano makubwa akiwa ndani ya La Masia, Barka alikuwa tayari ameshaanza kuandika jina lake nchini Hispania.

Safari yake ilianza kuonekana zaidi mwaka 2021 alipokuwa na umri wa miaka saba, aliposhiriki kliniki za vijana za akademi ya Ajax Amsterdam nchini Uholanzi.

BAR 02

Baadaye alijiunga na CF Damm, akademi iliyopo Catalonia, ambako ndipo kipaji chake kilipoanza kuzungumzwa zaidi.

Katika msimu wake wa mwisho akiwa Damm, Barka alifunga mabao 41 katika mechi 28 za ligi ya vijana, akimaliza akiwa kinara wa ufungaji.

Miongoni mwa michezo iliyoweka jina lake kwenye ramani ni ule dhidi ya vijana wa Barcelona, ambapo alifunga hat-trick. Kiwango hicho kikaanza kuwafanya viongozi wa Barcelona kumfuatilia kwa karibu.

BAR 03

Kabla ya kutua La Masia, Barka pia alichaguliwa katika kikosi bora cha vijana chini ya miaka 12 cha Shirikisho la Soka la Catalonia, baada ya kufunga mabao 18 katika mechi 20 za ligi.

Juni 2026, Barcelona ikampa nafasi ya kujiunga na akademi yake maarufu ya La Masia, hatua iliyomfanya kuwa Mtanzania wa kwanza kuingia katika mfumo huo wa klabu hiyo.

Hiyo ilikuwa hatua kubwa kwa kinda huyo ambaye sasa anaendelea kujifunza ndani ya moja ya mifumo maarufu zaidi ya kukuza vipaji iliyotoa mastaa wakubwa ulimwenguni kama Lionel Messi, Lamine Yamal na wengineo.